Iran yaalani mashambulizi ya kigaidi katika Jamhuri ya Dagestan, Russia
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyojiri katika Jamhuri ya Dagestan na kutoa mkono wa pole kwa taifa la Russia na serikali ya nchi hiyo khususan familia za wahanga wa jinai hiyo.
Kuhani na polisi wasiopungua 15 wameuawa baada ya watu waliokuwa na silaha kushambulia kanisa la Kiorthodox na kituo cha polisi katika miji miwili ya Makhachkala na Derbend huko Kafkazi ya kaskazini.
Kanaani ametaja kila aina ya ugaidi kuwa ni tishio kwa jamii ya mwanadamu na usalama wa dunia.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amewatakia ahueni ya haraka majeruhi wa mashambulizi hayo ya kigaidi katika Jamhuri ya Dagestan huko Russia na kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inauchukulia ugaidi wa aina zote kuwa tishio kwa jamii ya mwanadamu na usalama wa dunia.
Nasser Kanaani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza juu ya azma madhubuti na athirifu ya jamii ya kimataifa ili kukabiliana na tishio hilo la pamoja dhidi ya binadamu.