Jun 24, 2024 11:19 UTC
  • Borrell: Hali ya mambo ya Gaza haielezeki kufuatia mashambulizi ya Israel

Josep Borrel Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa hali ya mambo katika Ukanda wa Gaza ambako Israel inaendeleza mashambulizi yake ya mauaji ya unati tangu Oktoba mwaka jana haielezeki.

Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Umoja wa Ulaya la Mambo ya Nje, Josep Borrell amesema kuwa anasikitishwa na vifo vya Wapalestina zaidi ya 100 waliouawa katika mashambulizi ya karibuni ya utawala wa Israel. Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ametaja mauaji hayo dhidi ya Wapalestina kuwa ni moja ya siku iliyoshuhudia umwagaji damu mkubwa." 

Mauaji ya kimbari ya Wapalestina Ukanda wa Gaza 

Borrell amesema kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kuunga mkono mapendekezo ya kufikiwa mapatano ya kusimamisha vita Ukanda wa Gaza ambayo yatapelekea kufikishwa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo la sivyo hali ya mambo itazorota zaidi. 

Utawala wa Kizayuni umewaua shahidi Wapalestina zaidi ya 37,500 wengi wao wakiwa wanawake na watoto tangu uanzishe mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa eneo mwezi Oktoba mwaka jana.  

 

Tags