Jun 27, 2024 12:40 UTC
  • Waziri Mkuu: Norway kupokea wagonjwa kutoka Gaza

Jonas Gahr Store Waziri Mkuu wa Norway amethibitisha leo kuwa nchi hiyo itawapokea na kuwatibu Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza. Amesema Norway itashiriki katika juhudi za kimataifa za kuwasaidia Wapalestina ambao matibabu haraka iwezekanavyo.

Waziri Mkuu wa Norway amebainisha haya leo Alhamisii baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Umoja wa Ulaya (EU) kwa pamoja kueleza kuwa Wapalestina elfu 9 wanahitaji msaada wa haraka wa matibabu wa kupelekwa nje ya nchi hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu kufuatia mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya Gaza. 

Mbali na kuwatibu raia hao wa Palestina, Norway pia itatoa ndege ambazo zitawasafirisha wagonjwa wa Kipalestina katika nchi nyingine kwa ajili ya matibabu. Waziri Mkuu wa Norway amesema, kwa kufanya hivi tunaweza kutoa mchango wa kusaidia watu wengi kuliko uwezo tulio nao wa kupokea nchini kwetu kwa ajili ya matibabu." 

Norway kuwatibu majeruhi wa vita wa Gaza 

Hali ya binadamu katika Ukanda wa Gaza ni mbaya sana. Mfumo wa afya umesambaratika.  Itakumbukwa kuwa mwezi uliopita Norway iliitambua rasmi Palestina kama nchi. Ripoti za karibuni zinaonyesha kuwa hii leo ni hospitali 12 tu kati ya 35 katika Ukanda wa Gaza zinazofanya kazi kwa upande mmoja. 

 

Tags