Yair Golan: Vita vya Gaza lazima visitishwe haraka iwezekanavyo
Mkuu wa Chama cha Kidemokrasia cha utawala wa Kizayuni wa Israel ametaka kusimamishwa vita haraka iwezekanavyo dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.
Yair Golan amesema hali ya Gaza ni maafa yasiyo ya kawaida na ametaka kusitishwa vita haraka katika eneo hilo.
Gazeti la Kizayuni la Haaretz limeandika kuwa: Mkuu wa Chama cha Kidemokrasia amesema kile wanachokishuhudia hii leo huko Gaza ni maafa yasiyo ya kawaida na kwamba vita ni lazima visimamishwe mara moja.
Golan ameongeza kuwa, baraza la mawaziri la Netanyahu linapinga kubadilisha hatua kijeshi zilizochukuliwa kuwa hatua ya kisiasa kwa ajili ya kuimarisha usalama wa Israel.
Mwanasiasa huyo wa Israel ameongeza kuwa: Njia ya ufumbuzi ya serikali mbili ndio njia bora zaidi ya ufumbuzi wa kiusalama na kitaifa kwa ajili ya Israel, hata hivyo leo hii tumekumbwa na mshtuko.
Golan amesema pia kwamba mpango wa kutaka kuliunganisha eneo la Ukingo wa Magharibi na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) utakuwa wa maafa.
Jeshi la utawala wa Kizayuni hivi karibuni lilizidisha mashambulizi yake dhidi ya taasisi za kiraia na kambi za wkaimbizi wa Kipalestina huko Ukanda wa Gaza.