Waislamu wa Nigeria washerehekea ushindi wa Iran dhidi ya Marekani na Israel
(last modified Wed, 25 Jun 2025 08:57:23 GMT )
Jun 25, 2025 08:57 UTC
  • Waislamu wa Nigeria washerehekea ushindi wa Iran dhidi ya Marekani na Israel

Waislamu nchini Nigeria wamesherehekea ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya Marekani na utawala haramu wa Israel baada ya vita kati ya Iran na Isreal kusitishwa baada ya kudumu kwa siku 12.

Ripoti zinasema kuwa, maadhimisho ya sikukuu za Eidul-Ghadir na Mubahala ziligeuka kuwa sherehe za Iran nchini Nigeria ambapo Waislamu walishangilia ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vita vya siku 12 vya kukabiliana na uchokozi wa Israel na Marekani dhidi ya Iran.

Katika miji mingi ya Nigeria, Eid Ghadir haikufanyika tarehe 18 Dhul-Hijjah kama ilivyo ada, badala yake, ummah wa Kiislamu hasa wafuasi wa Ahlulbayt, waliandaa dua na maombi kwa ajili ya Iran juu ya vita na madola ya kibeberu ya dunia.

Katika mji mkuu wa Abuja nchini Nigeria, mamia ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wakati wa sherehe za pamoja za Ghadir na Eid Mubahala walishangilia ushindi wa Iran. Waislamu haohekea hao waliimba nara za kuunga mkono Iran na kuwalaani Marekani na Israel. Pia wamesisitiza utiifu wao kwa Imam Mahdi, Mwokozi Aliyeahidiwa, na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei.

Zaidi ya hayo, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky pia aliongoza marasimu kama hayo huko Abuja ambayo yalikuwa na mahudhurio makubwa ya watu.