Iran yasisitisha ushirikiano wake na wakala wa IAEA
Wawakilishi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu wameidhinisha vipengee vikuu na vidogo vya mpango wa kuitaka serikali kusitisha ushirikiano wake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
Katika kikao chao cha leo, Wabunge waliohudhuria kikao wamepasisha mpango huo kwa kura 221 za ndio, moja ya kujizuia na kutokuweko kura ya hapana.
Seyyed Mahmoud Nabaviyan, mwakilishi wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa, amesema kuwa mada ya mpango huu sio kujiondoa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mkataba wa NPT na kusema: "Tunafungamana na mkataba huu na tumeutangazia ulimwengu kwamba shughuli zetu zote za nyuklia zimekuwa ni za amani. Kwa hivyo, mpango huu unashughulikia suala la ushirikiano na Wakala wa kimataifa wa IAEA, ikimaanisha kuwa uwekaji wa kamera katika taasisi zetu utapigwa marufuku.
Wakati huo huo, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu sambamba na kubainisha kwamba, hatutadanganywa na ahadi zozote na tutakuwa tayari zaidi kuliko hapo awali kubonyeza kitufe cha kufyatua risasi na kutoa jibu kali kwa uchokozi wowote ameeleza kuwa: "Mpango wa nyuklia wa amani wa Iran utasonga mbele kwa kasi kubwa."