Jun 27, 2024 06:26 UTC

Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vimesambaza video na picha zinazoonyesha kombora la balestiki la hypersonic la vikosi majeshi ya nchi hiyo lililotumika kupiga meli ya utawala wa Kizayuni katika Bahari Nyekundu au Bahari ya Sham.

Msemaji wa jeshi la Yemen amesema kuwa kombora hilo linaitwa "Hatem-2" na ndilo lililotumika kupiga meli ya Israel ya "MSC SARAH V."

Taarifa iliyoambatanishwa na video hiyo imesema kwamba, hii ni mara ya kwanza kwa majeshi ya Yemen kusambaza video kama hiyo. 

Msemaji wa Jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema kuwa, kombora hilo limezalishwa na wananchi wenyewe wa Yemen na linatumia teknolojia ya kisasa, linapiga shabaha kwa umakini wa hali ya juu, na uteketezaji wake ni mkubwa.

Sambamba na maelezo haya tumeweka video na picha kuhusu kombora hilo.

 

Tags