Jun 27, 2024 06:11 UTC
  • Balozi wa utawala wa Kizayuni aitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi, kuhusu ujasusi dhidi ya mahakama ya ICC

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Uholanzi imesema imemwita wizarani humo balozi wa utawala ghasibu wa Israel baada ya kuchapishwa habari kuhusu uwezekano wa kupenya Wazayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya mjini Hague.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Uholanzi imetangaza katika taarifa kwamba, imemuita wizarani humo Modi Ephraim, balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ili afafanue kuhusu hatua za utawala wa Kizayuni za kufanya ujasuzi, kutoa vitisho na kudukua kompyuta za Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) huko mjini The Hague.

Ikiwa ni nchi mwenyeji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai mjini Hague, pamoja na nchi nyingine 93 duniani, Uholanzi ina jukumu kulinda usalama wa mahakama hiyo ya Kimataifa na wafanyakazi wake.

Karim Khan

Karim Khan, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, alitangaza mwezi Mei 20, 2024, kwamba mahakama hiyo inafuatilia kutolewa hati ya kukamatwa Benjamin Netanyahu na "Yaoav Galant Waziri Mkuu na Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni. Kuhusiana na hilo, ujumbe wa majaji wa Mahakama ya Kimataifa unatakiwa kuchunguza ombi hilo la Karim Khan.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC); ametangaza mashtaka yanayowakabili Netanyahu na Gallant kuwa ni mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina, kusababisha njaa kama njia ya vita, kuzuia misaada ya kibinadamu kufika Ukanda wa Gaza na kuwalenga kwa makusudi raia wasio na hatia katika operesheni zake za kijeshi kwenye ukanda huo.

Tags