Jun 29, 2024 11:47 UTC
  • Wazayuni washambulia mahema ya wakimbizi wa Kipalestina kusini mwa Gaza

Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel waliokuwa wamejizatiti kwa vifaru wamevamia mahema ya wakimbizi wa Kipalestina katika eneo la al Mawasi kaskazini magharibi mwa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Wapalestina 11 wameuawa shahidi na zaidi ya 40 wamejeruhiwa katika ufyatuaji risasi wa kushtukiza uliofanywa na wanajeshi wa Kizayuni katika eneo la al Mawasi magharibi mwa Rafah. 

Vilevile Wapalestina wengine 4, wakiwemo watoto 2, wameuliwa shahidi na 10 kujeruhiwa baada ya ndege za kivita za Israel kushambulia nyumba moja katika mtaa wa al Wahda katikati mwa mji wa Gaza. 

Shambulio la Wazayuni katika mtaa wa al Wahda katikati mwa mji wa Gaza 

Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimeishambulia nyumba nyingine katika eneo la wakimbizi ya al Maghazi katikati mwa Ukanda wa Gaza. 

Jana Ijumaa pia ndege za kivita za Israel ziliyashambulia maeneo kadhaa ya Ukanda wa Gaza na kuuwa shahidi Wapalestina 21 na kujeruhi makumi ya wengine.  

Wakati huo huo, wanamapambano wa Palestina wamewaangamiza wanajeshi 9 wa Kizayuni katika mapigano makali huko Shujaiya mashariki mwa mji wa Quds. 

Tags