Njaa yaenea Gaza kutokana na kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i113318-njaa_yaenea_gaza_kutokana_na_kuendelea_mashambulizi_ya_utawala_wa_kizayuni
Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza amesisitiza kuwa njaa inazidi kuongezeka katika keneo kila siku kufuatia kushtadi mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa ukanda huo.
(last modified 2024-06-25T04:14:24+00:00 )
Jun 25, 2024 04:14 UTC
  • Njaa yaenea Gaza kutokana na kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni

Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza amesisitiza kuwa njaa inazidi kuongezeka katika keneo kila siku kufuatia kushtadi mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa ukanda huo.

Ismail al-Thawabateh ameeleza kuwa utawala wa Kizayuni umekiuka sheria za kimataifa kwa kukidhibiti kivuko cha Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza, kukichimba na kukichoma moto. Amesema wagonjwa elfu 25 wameshindwa kutoka Gaza na kwenda nje kwa ajili ya matibabu baada ya utawala wa Kizayuni kukichoma kivuko cha Rafah. 

Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza ameongeza kuwa: Malori elfu 15 ya misaada ya kibinadamu yamekwama hivi sasa kufuatia kufungwa  vivuko vya Rafah na Karam Abu Salem. 

Wakazi wa Ukanda wa Gaza na mateso ya njaa

Wizara ya Afya ya Gaza imetoa taarifa na kuripoti kuwa Wapalestina 94 wameuawa shahidi na kujeruhiwa katika jinai za jana usiku za jeshi la utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza. Imesema kuwa, hadi sasa Wapalestina elfu 7,626 wameuawa shahidi na elfu 86 na 98 kujeruhiwa tangu israel ianzisha mashambulizi ya kikatili na mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza Oktoba mwaka jana.