Jun 27, 2024 12:42 UTC
  • Waandamanaji Kenya wamtaka Rais Ruto ajiuzulu licha ya kuurejesha muswada wa fedha bungeni

Waandamanaji Kenya wanamtaka Rais wa nchi hiyo William Ruto ajiuzulu licha ya uamuzi wake wa kuuondoa muswada tata wa fedha wa 2024 uliokuwa umedhamiria kuongeza ushuru ili kusaidia kupunguza mzigo wa madeni nchini humo.

Muswada huo umeibua maandamano makubwa ya Wakenya ambapo polisi jana juzi Jumatano walikabiliana na wanadamanaji ambapo watu wasiopungua 23 waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi. 

Polisi leo waliweka vizuizi barabarani katika mitaa inayoelekea katika ikulu ya Rais huku baadhi ya waandamanaji wakiahidi kuidhibiti ikulu licha ya Rais Ruto kuuweka kando muswada wa fedha wa 2024 ulioibua maandamano kote nchini humo kwa wiki sasa. 

Baadhi ya waandamanaji wameeleza kuwa malengo yao yamefanikiwa na kwamba leo wasingeshiriki maandamanoni. Kundi jingine la waandamaji limeahidi kusongambele na maandamano yao wakisema kuwa hatua itakayowaridhisha ni kuondoka mamlakani Rais Ruto. 

Rais William Ruto wa Kenya 

Rais wa Kenya anakabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi uliogubika uongozi wake wa miaka miwili; ambapo vijana nchini humo wanaongoza maandamano makubwa ya kupinga ongezeko la ushuru huku wakisisitiza kutekelezwa mageuzi makubwa ya kisiasa. 

Tags