Jun 27, 2024 08:07 UTC

Wapiganaji wa Hizbullah ya Lebanon kwa mara nyingine tena wamelenga na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa katika maeneo ya wanajeshi wa Kizayuni kwenye mpaka wa nchi hiyo na Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ilitangaza katika taarifa siku ya Jumatano kwamba, ikiwa ni katika kuunga mkono taifa la muqawama la Palestina katika Ukanda wa Gaza na kujibu hujuma za adui Mzayuni dhidi ya vijiji vya Lebanon, wapiganaji wake wamelenga kwa sihala zinazofaa jengo ambalo jeshi la Kizayuni lilikuwa limekusanyika ndani yake kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Hizbullah imeongeza katika taarifa hiyo kwamba idadi kubwa ya Wazayuni waliuawa au kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Wapiganaji wa muqawama wa Kiislamu wa Lebanon pia waliharibu vifaa vya kijasusi karibu na kambi ya Barke Risha jana mchana kwa kutumia silaha zinazofaa.

Athari za mashambulio ya Hizbullah ya Lebanon kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu

Kufuatia kutekelezwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na muqawama wa Palestina wa Ukanda wa Gaza dhidi ya vikosi vya Wazayuni vinavyokalia kwa mabavu ardhi ya Palestina, muqawama wa Kiislamu wa Lebanon pia ulianzisha operesheni kubwa dhidi ya wavamizi wa Kizayuni kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa lengo la kupunguza sehemu ya nguvu za kijeshi za utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimekiri kuhusu mapigo makubwa yanayotolewa na wapiganaji wa muqawama wa Kiislamu wa Lebanon dhidi ya eneo la kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kusema, operesheni za Hizbullah zimesababisha uharibifu mkubwa dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika eneo hilo.

Hatua ya Hizbollah ya kutumia silaha za hali ya juu na za kisasa kabisa dhidi ya maeneo nyeti ya utawala ghasibu wa Israel imeibua hofu na wasiwasi mkubwa miongoni mwa maghasibu hao wa Quds Tukufu na kupelekea maelfu kwa maelfu ya walowezi wa Kizayuni kukimbia vitongoji vyao kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya kijeshi wa utawala wa Kizayuni, Hizbullah ya Lebanon pekee imeshughulisha nusu ya uwezo wa kijeshi wa utawala huo katika upande wa kaskazini na kuzuia kuwepo kwa nguvu jeshi hilo vamizi katika eneo la kusini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Tags