Jun 23, 2024 07:37 UTC
  • Jibu la Hizbullah litaurejesha utawala wa Israel katika Zama za Mawe

Kituo cha Taarifa za Vita cha Hizbullah ya Lebanon kimetangaza kuwa, shambulio kali la harakati hiyo ya muqawama dhidi ya vituo nyeti vya utawala wa Kizayuni, ambavyo vinajulikana tu na vyombo vya usalama vya utawala huo, litairejesha Israel katika zama za mawe.

Katika siku za hivi karibuni, utawala wa Kizayuni kwa kushadidisha mashambulizi yake ndani kabisa ya Lebanon, umeitishia nchi hiyo na muqawama wa Hizbullah kuwa utaongeza mashambulizi yake dhidi ya nchi hiyo kutokana na hatua ya harakati hiyo ya kuunga mkono muqawama wa wananchi wa Palestina.

Unyama wa wanajeshi wa utawala Israel dhidi ya Wapalestina

Ikiwa ni katika kujibu vitisho vya hivi karibuni vya utawala wa Kizayuni vya kuishambulia Lebanon, Kituo cha Tarifa za vita cha Hizbullah ya Lebanon karibuni kimerusha hewani picha za video za vituo nyeti vya kijeshi na kiusalama vya utawala haramu wa Israel, zenye maandishi ya Kiingereza na Kiebrania, ambazo zimepigwa na droni za Hizbullah tokea angani zikiwa na maelezo sahihi, ndani kabisa ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.

Kituo hicho kimesisitiza kuwa picha hizo ni za vituo nyeti za utawala wa Kizayuni, ambavyo ni vyombo vya usalama vya utawala huo pekee ndivyo vinavifahamu, na kuwa kushambuliwa kwake kutairejesha Israel katika zama za mawe.

Mwanzoni mwa picha hizo, kuna maneno ya Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, ambaye alisema karibuni, kwamba ikiwa Lebanon italazimishwa kupigana vita, Hizbullah itapigana vita kwa nguvu zake zote na bila kuzingatia kanuni wala viwango vyo vyote.

Mwishoni mwa video hiyo, kuna sehemu nyingine ya maneno ya Sayyid Hassan Nasrallah akisema: 'Mtu yeyote anayepanga vita dhidi yetu atajuta,  Inshaallah."

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vya Hizbullah, picha hizo zina ujumbe ambao ni wachukua maamuzi wa Israel pekee ndio wanauelewa vizuri na kuwa ni onyo rasmi la Hizbullah dhidi ya makao makuu ya Wizara ya Vita huko Tel Aviv.

Tags