-
Maelfu waandamana kote Ulaya kuunga mkono Palestina, kulaani ukatili wa Israel
Feb 01, 2026 10:32Waelfu kwa maelfu ya watu wamejitokeza mitaani katika nchi kadhaa za Ulaya kushiriki maandamano ya kuunga mkono Palestina, huku wakiushutumu utawala wa Israel kwa kukiuka mara kwa mara makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza kati yake na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas.
-
Sera za uadui za Umoja wa Ulaya dhidi ya Iran; Brussels inataka nini?
Jan 31, 2026 08:57Umoja wa Ulaya umeendeleza msimamo wake wa kuingilia masuala ya ndani ya Iran kwa kuweka vikwazo vipya dhidi ya Tehran kwa kisingizio cha masuala ya haki za binadamu.
-
Katibu Mkuu wa NATO: Ulaya 'iendelee kuota' kama inadhani inaweza kujilinda bila ya US
Jan 27, 2026 06:38Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte amesema, Umoja wa Ulaya, EU bali hata Ulaya nzima haina uwezo wa kujilinda bila ya Marekani na kusisitiza kuwa, nchi wanachama zitalazimika kutumia hadi 10% ya Pato lao la Taifa kwa ajili ya shirika hilo la kijeshi, ambayo inaweza pia isitoshe.
-
Orban: Hungary haitaruhusu Ukraine kujiunga na EU miaka 100 ijayo
Jan 24, 2026 02:47Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban amesema kwamba Ukraine inajaribu kushawishi na kuathiri matokeo ya uchaguzi ujao wa bunge nchini Hungary, akisitiza kuwa nchi yake haitaruhusu Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya katika miaka 100 ijayo.
-
Bunge la EU lasimamisha makubaliano ya biashara na US; kisa vitisho vya Trump
Jan 22, 2026 05:51Bunge la Ulaya limesimamisha rasmi mchakato wa kuidhinisha makubaliano yake ya kibiashara na Marekani, kutokana na vitisho vya Rais Donald Trump vya kutoza ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za EU zinazoenda Marekani, iwapo umoja huo hautaafiki azma ya Washington ya kuitwaa Greenland.
-
"Haiwezi Tena Kuvumilika", asema Waziri Mkuu wa Ubelgiji akiitaka Ulaya iamue moja kuhusu Trump
Jan 21, 2026 10:39Waziri Mkuu wa Ubelgiji Bart De Wever amesema, ni lazima Ulaya imueleze wazi Rais wa Marekani Donald Trump kwamba hali ilipofikia hivi sasa "Haiwezi Tena Kuvumilika".
-
Russia: Badala ya Ulaya kuzungumzia hali ya Iran ifuatilie kuiokoa Greenland
Jan 15, 2026 10:27Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova amesema, badala ya viongozi wa Umoja wa Ulaya, EU kutoa matamshi ya kuzungumzia hali ya Iran, ingekuwa bora kama wanegejikita kushughulikia kadhia ya Greenland, ambayo sasa hivi Marekani inafanya juu chini kuitia mkononi.
-
Mkuu wa zamani wa Sera za Nje wa EU: Ulaya iache kuifanya Marekani muitifaki wake mkuu
Jan 07, 2026 15:00Josep Borrell, mwanadiplomasia mkuu wa zamani wa Umoja wa Ulaya (EU) amesema, kambi hiyo inapaswa iache kuichukulia Marekani kama mshirika wake mkuu, huku Washington na Brussels zikiwa zinazozana hivi sasa kuhusu sera za kidijitali na udhibiti wa eneo la Greenland.
-
Baraza la Makanisa Duniani lataka kuwekewa vikwazo Israel kutokana na vita vya Gaza
Jan 02, 2026 02:48Baraza la Makanisa Duniani (WCC) limeutaka Umoja wa Ulaya (EU) kuiwekea Israel vikwazo vikiwemo vya silaha kutokana na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni huko Gaza, na ukiukaji wa haki dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.
-
WHO: Unywaji wa pombe unaua watu 800,000 kila mwaka Ulaya
Dec 28, 2025 06:35Unywaji wa pombe unasababisha vifo vya watu zaidi ya 800,000 kila mwaka barani Ulaya, na kusababisha kifo kimoja kati ya kila vifo kumi na moja, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO).