Pars Today
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeyaweka maeneo manane ya kihistoria ya kabla ya ujio wa Uislamu hapa nchini Iran katika orodha yake ya turathi za dunia.
Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zimetengwa kimataifa bada ya kutangaza kujiondoa katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO.
Marekani imetangaza kuwa itajiondoa kwenye Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kuanzia Disemba 31 mwaka huu.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limetangaza kuwa, watoto wapatao milioni 1.8 wamenyimwa fursa ya kusoma katika nchi ya Sudan Kusini kutokana na hali mbaya ya vita na ukosefu wa amani.
Leo Septemba nane ni siku ya kimataifa ya kupinga ujinga wa kutojua kusoma na kuandika ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni 'kusoma na kuandika katika dunia ya kidijitali'.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limeuweka mji wa al Khalil na Haram ya Nabii Ibrahim (as) katika orodha ya turathi za kimataifa zinazokabiliwa na hatari ya kutoweka na limelaani vikali hatua za utawala ghasibu wa Israel katika eneo hilo.
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kuunga mkono mapambano ya wananchi wa Palestina na hakuna wakati ambao Tehran ilisitisha himaya na uungaji mkono wake huo.
Wito uliotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kikao cha Shirika la Elimu, Syansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) wa kunyamaza kimya dakika moja ili kuonesha heshima kwa eti wahanga wa mauaji ya Holocaust umekabiliwa na upinzani mkali wa mwakilishi wa Cuba katika kikao hicho.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limelaani vikali hatua ya kundi la kigaidi la Daesh ya kubomoa Msikiti wa kihistoria wa al Nuri katika mji wa Mosul nchini Iraq.
Kamati ya Utendaji ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Utamaduni na Sayansi UNESCO Jumanne ilipitisha azimio ambalo liliulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kukiuka sheria za kimataifa katika mji wa Quds (Jerusalem) na Ukanda wa Ghaza.