-
Israel yakiri, Hizbullah imetungua ndege yake isiyo na rubani
Sep 09, 2019 06:56Duru zenye mfungamano na utawala wa Kizayuni wa Israel zimethibitisha kuwa, wapiganaji wa Hizbullah ya Lebanon wametungua ndege isiyo na rubani ya utawala huo.
-
Sisitizo la Corbyn la kukabiliana na muungano wa Netanyahu na Trump dhidi ya JCPOA
Sep 07, 2019 01:50Tangu yalipofikiwa makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) mwaka 2015, Marekani na utawala wa Kizayuni zimekuwa zikisisitiza kila mara kuwa zinayapinga makubaliano hayo na kutaka yavunjwe. Na katika hatua iliyolenga kufikia lengo hilo, mwezi Mei 2018, Rais Donald Trump wa Marekani alitangza kujitoa nchi yake kwenye makubaliano hayo na kuanza kutekeleza vikwazo vikali ambavyo havijawahi kushuhudiwa dhidi ya Iran.
-
Malengo ya safari ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni huko Al Khalil
Sep 06, 2019 01:34Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel Septemba Nne, kwa mara ya kwanza alifika katika mji wa Al Khalil (Hebron) katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kisha akaingia katika msikiti maarufu wa Masjid Ibrahimi katika mji huo. Kabla ya safari hiyo ya Netanyahu, rais wa utawala wa Kizayuni Reuven Rivlin naye pia alifika katika mji wa Al Khalil na kutembelea Masjid Ibrahimi.
-
EuroMed Rights yatoa wito wa kukabiliana na jinai za Israel
Sep 05, 2019 06:38Jumuiya ya Kutetea Haki za Binadamu Ulaya na Miditerania (EuroMed Rights) imelitaka Bunge la Uswisi lisisalimu amri mbele ya mashinikizo ya utawala wa Kizayuni wa Israel yanayolitaka lisipasishe sheria ya kuwakamata maafisa waliohusishwa na jinai za kivita dhidi ya Wapalestina.
-
Baqeri: Utawala wa Kizayuni unazidi kudhoofika
Sep 05, 2019 00:04Mkuu wa Kamandi ya Vikosi Vyote vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Kambi ya muqawama (mapambano ya Kiislamu) inazidi kusonga mbele katika kuudhoofisha utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo."
-
Ripota wa UN: Matatizo ya ukosefu wa amani Nigeria yapewe mazingatio
Sep 03, 2019 03:37Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa matatizo ya kiusalama ya Nigeria yametengeneza mgogoro ambao unahitajia kupewa mazingatio haraka iwezekanavyo, la sivyo utasababisha ukosefu wa usalama katika nchi nyingine za Kiafrika.
-
Mahakama ya ICC yamtaka Bensouda achunguze tena shambulizi la Israel dhidi ya meli ya Marmara
Sep 03, 2019 03:23Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetaka kufanyike tena uchunguzi kuhusu shambulizi lililofanywa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya meli ya Marmara ya Uturuki iliyokuwa na misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Ukanda wa Gaza hapo mwaka 2010.
-
"Israel haina uwezo wa kukabiliana na wanamapambano wa Kiislamu"
Sep 02, 2019 03:12Mtandao maarufu wa habari unaotembelewa na watu wengi nchini Ugiriki umetoa ripoti maalumu na kusema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel hauna uwezo wa kukabiliana na wanamapambano wa Kiislamu wa Hizbullah ya Lebanon.
-
Al Manar: Kamanda wa jeshi la utawala wa Kizayuni aangamizwa kwenye oparesheni ya Hizbullah ya Lebanon
Sep 01, 2019 12:46Televisheni ya al Manar imetangaza kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeangamiza moja ya zana za kijeshi za Israel katika barabara ya al Thakna katika mji wa mpakani wa Israel wa Avivim na kumuua kamanda wa kikosi kimoja wa jeshi la utawala wa Kizayuni huko kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu katika oparesheni iliyotekelezwa na harakati ya Hizbullah.
-
Makampuni ya Imarati yanunua ardhi za mji wa Quds kwa ajili ya Wazayuni
Aug 29, 2019 03:22Naibu Mwenyekiti wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina amesema kuwa makampuni ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) yananunua ardhi huko Quds na kisha kukabidhi umiliki wa ardhi hizo kwa Waisraeli.