EuroMed Rights yatoa wito wa kukabiliana na jinai za Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i55813-euromed_rights_yatoa_wito_wa_kukabiliana_na_jinai_za_israel
Jumuiya ya Kutetea Haki za Binadamu Ulaya na Miditerania (EuroMed Rights) imelitaka Bunge la Uswisi lisisalimu amri mbele ya mashinikizo ya utawala wa Kizayuni wa Israel yanayolitaka lisipasishe sheria ya kuwakamata maafisa waliohusishwa na jinai za kivita dhidi ya Wapalestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 05, 2019 06:38 UTC
  • EuroMed Rights yatoa wito wa kukabiliana na jinai za Israel

Jumuiya ya Kutetea Haki za Binadamu Ulaya na Miditerania (EuroMed Rights) imelitaka Bunge la Uswisi lisisalimu amri mbele ya mashinikizo ya utawala wa Kizayuni wa Israel yanayolitaka lisipasishe sheria ya kuwakamata maafisa waliohusishwa na jinai za kivita dhidi ya Wapalestina.

Shirika hilo la ulaya la kutetea haki za binadamu limeeleza wasiwasi wake kuhusu safari ya ujumbe wa Israel nchini Uswisi na kusema kuwa, lengo ya safari hiyo ni kuzuia upasishaji wa sheria inayoiruhusu serikali ya Uswisi kuwatia nguvuni maafisa wa kisiasa na kijeshi wa Israel wanautuhumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuwa wamefanya jinai za kivita. 

Mbali na Bunge la Uswisi, taarifa ya jumuiya hiyo imewataka maafisa wa taasisi nyingine za nchi hiyo kushikamana na msimamo wao wa kufuatilia kisheria uhalifu na jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya raia wa Palestina.

Wapalestina wanaendelea kuuawa kinyama

EuroMed Rights pia imezitaka nchi nyingine za Ulaya kufuata nyayo za Uswisi na kutunga sheria zinazoziwezesha mahakama za nchi hizo kuwatia nguvuni na kuwahukumu maafisa wa Israel waliofanya jinai na ukatili dhidi ya Wapalestina. 

Maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya utawala wa Kizayuni wa Israel wamekuwa wakiogopa kufanya safari nchini Uswisi wakihofia kutiwa nguvuni kutokana na kuhusikwa kwao na jinai na mauaji ya raia wa Palestina.