-
Rais wa Sudan Kusini atuhumiwa kwa upendeleo baada ya kumteuwa binti yake katika cheo cha juu serikalini
Aug 27, 2025 07:10Adut Salva Kiir, binti wa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ameteuliwa na baba yake kuwa Mjumbe wa Rais Anayehusika na Mipango Maalumu, kazi ambayo awali ilikuwa inafanywa na Makamu wa Rais wa sasa.
-
Ufaransa yarejesha mafuvu ya vichwa Madagascar miaka 127 baada ya mauaji ya kikoloni
Aug 27, 2025 03:29Ufaransa jana Jumanne ilirejesha mafuvu matatu nchini Madagascar, likiwemo moja linaloaminika kuwa la mfalme aliyekatwa kichwa na wanajeshi wa Ufaransa kufuatia mauaji ya Agosti 1897.
-
Baraza la Mawaziri Sudan lafanya kikao cha kwanza mjini Khartoum tangu 2023
Aug 27, 2025 03:28Baraza la Mawaziri la Sudan ya Sudan lilifanya mkutano wake wa kwanza katika mji mkuu, Khartoum, jana Jumanne tangu kuzuka kwa vita vya ndani nchini humo katikati ya Aprili, 2023.
-
Mrengo wa upinzani Somalia wafikia makubaliano na serikali kuhusu uchaguzi
Aug 26, 2025 22:58Mrengo uliojitenga na muungano mkuu wa upinzani nchini Somalia wa Salvation Forum umetia saini makubaliano ya uchaguzi na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, na hivyo kutoa pigo kubwa kwa harakati kuu ya upinzani nchini humo.
-
Ugonjwa wa kipindupindu wauwa watu 63 mashariki mwa Chad
Aug 26, 2025 22:57Watu wasiopungua 63 wamepoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu katika jimbo la Ouaddai mashariki mwa Chad tangu katikati ya mwezi Julai mwaka huu. Taraifa hii imetolewa na Wizara ya Afya ya nchi hiyo.
-
Rais wa Rwanda akadhibisha ripoti zinazolihusisha jeshi na mauaji mashariki mwa Kongo
Aug 26, 2025 11:42Rais Paul Kagame wa Rwanda amekadhibisha ripoti kwamba jeshi la nchi hiyo lilihusika katika mauaji mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Botswana yatangaza dharura ya kiafya huku kukiwa na uhaba mkubwa wa dawa
Aug 26, 2025 11:31Botswana imetangaza dharura ya kiafya huku nchi hiyo ikikabiliwa na upungufu mkubwa wa dawa na vifaa tiba. Uhaba huo umesababisha hospitali na zahanati nchini humo kuhangaika kutibu magonjwa kuanzia shinikizo la damu, kisukari hadi saratani.
-
Pigo jingine kwa Mpango wa Abraham; Kwa nini Libya inapinga uhusiano wa kawaida na Israel?
Aug 26, 2025 08:33Serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya imekataa nchi hiyo kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Maafisa wa jeshi la DR Congo wasailiwa huku mapigano yakishadidi eneo la mashariki
Aug 26, 2025 02:30Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilitangaza Jumatatu kwamba maafisa 41 wa ngazi za juu jeshini wamesailiwa kama sehemu ya uchunguzi kuhusu kushindwa kwa vikosi vya serikali wakati wa mapigano dhidi ya waasi wa M23 katika eneo la mashariki la nchi hiyo lenye machafuko.
-
UN yataka nchi za Afrika zishirikiane kijeshi ili kudumisha amani
Aug 26, 2025 02:28Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina J. Mohammed, amewataka viongozi wa kijeshi wa Afrika kushirikiana kwa karibu zaidi ili kukabiliana na ongezeko la vitisho vya usalama, ugaidi na athari za mabadiliko ya tabianchi katika bara hilo.