WHO: Wagonjwa wa kipindupidu Sudan wafikia 113,500; chanjo yaendelea kutolewa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i131150-who_wagonjwa_wa_kipindupidu_sudan_wafikia_113_500_chanjo_yaendelea_kutolewa
Shirika la Afya Duniani leo Jumanne limetangaza kuwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umewaathiri watu zaidi ya 113,600 na kuuwa zaidi ya 3,000 kote nchini humo tangu Julai mwaka jana.
(last modified 2025-09-23T11:53:39+00:00 )
Sep 23, 2025 11:53 UTC
  • WHO: Wagonjwa wa kipindupidu Sudan wafikia 113,500; chanjo yaendelea kutolewa

Shirika la Afya Duniani leo Jumanne limetangaza kuwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umewaathiri watu zaidi ya 113,600 na kuuwa zaidi ya 3,000 kote nchini humo tangu Julai mwaka jana.

Hala Khudari Mwakilishi wa WHO huko Sudan amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kwamba mlipuko huo umesababisha vifo vya asilimia 2.7, huku Darfur ikitajwa kuwa eneo lililoathiriwa zaidi.

Tangu juzi Jumapili wagonjwa 12,739 wa kipindupindu na vifo 358 vimeripotiwa katika maeneo 36 kati ya 64 ya Darfur. Tawilah huko Darfur ya Kaskazini eneo ambalo lina jamii ya watu zaidiya laki tano inawakilisha asilimia 61 ya kesi zote katika jimbo hilo.

Kampeni ya utoaji chanjo ya kipindupindu ilianza juzi Jumapili. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Hala Khudari Mwakilishi wa WHO huko Sudan. Amesema chanjo hizo zikilenga kuwalinda watu milioni 1.86 katika maeneo sita hatarishi ya Darfur Kusini, Mashariki na Kaskazini. Chanjo zilitolewa mapema mwezi huu huko Nyala baada ya kucheleweshwa kwa wiki kadhaa kulikosababishwa na kukosekana chanjo na changamoto za kilojistiki.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) vinaendelea nchini Sudan tangu Aprili 2023, ambapo hadi sasa maelfu ya watu wameuawa na kujeruhiwa, sambamba na kuenea  magonjwa mbalimbali.