-
Mgomo wa madaktari Kenya wakaribia, muungano wake watoa siku 14 kwa serikali
Aug 07, 2025 08:26Sekta ya huduma za afya nchini Kenya, kwa mara nyingine inakabiliwa na mzozo baada ya Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno (KMPDU) kutoa notisi ya siku 14 ya mgomo kutokana na kile inachosema kutotiliwa maanani kwa makubaliano waliyotiliana saini kati ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti.
-
Je, Afrika Kusini inafanya nini kukabiliana na ushuru mpya wa kibiashara wa Marekani?
Aug 07, 2025 04:49Wizara ya Biashara ya Afrika Kusini imetangaza kuwa imechukua hatua kadaa mpya za kukabiliana na ushuru mpya wa kibiashara wa Marekani.
-
Mawaziri wa serikali na maafisa wa chama tawala wafariki dunia katika ajali ya helikopta ya jeshi Ghana
Aug 07, 2025 04:27Imeripotiwa kuwa ajali ya helikopta ya kijeshi iliyotokea jana nchini Ghana imeua watu wote wanane waliokuwa ndani chombo hicho ikiwa ni pamoja na mawaziri wa ulinzi na mazingira wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi na maafisa wengine wakuu wa serikali.
-
Mwakilishi wa Algeria UN: Operesheni za anga za msaada kwa watu wa Gaza hazifai
Aug 07, 2025 04:04Mwakilishi wa Algeria katiika Umoja wa Mataifa, Amar Bendjama, amesema kuhusu operesheni za anga za kupeleka misaada katika Ukanda wa Gaza kwamba: "Kurusha misaada ya kibinadamu kwa njia ya anga kwa watu wa Gaza peke yake hakuwezi kutatua mgogoro wa njaa katika eneo hilo na kwamba utawala vamizi wa Israel lazima afungue njia zote za vivuko, barabara na njia za kibinadamu ili kufikisha misaada kwa waathiriwa."
-
Hasira zatanda Sudan baada ya kukamatwa mamluki wa kigeni wanaowasaidia waasi wa RSF
Aug 07, 2025 00:59Mitandao ya kijamii ya Sudan imetawaliwa na ghadhabu kubwa baada ya Jeshi la Sudan kufichua kwamba mamluki wa kigeni, wakiwemo wapiganaji kutoka Colombia, wanapigana bega kwa bega na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mapigano ya hivi majuzi huko El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.
-
Ruto aijia juu Marekani kwa mpango wa kuiadhibu Kenya, kisa? kuwa na uhusiano na China
Aug 07, 2025 00:24Rais William Ruto wa Kenya amekemea vikali serikali ya Marekani kufuatia mpango wake wa kuchunguza uhusiano wa Kenya na China, akisisitiza kuwa ushirikiano wa kibiashara na taifa hilo la Asia ni kwa maslahi ya kitaifa ya Kenya.
-
Ethiopia yamteua Balozi mpya nchini Somalia baada ya miezi kadhaa ya mvutano wa kidiplomasia
Aug 06, 2025 08:58Balozi mpya wa Ethiopia nchini Somalia, Suleiman Dedefo, amewasilisha rasmi hati zake za utambulisho kwa Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, katika hatua inayoashiria kurejesha uhusiano wa kawaida baada ya miezi kadhaa ya mvutano wa kidiplomasia.
-
Rais wa Baraza la Uongozi Sudan: Tutapambana na RSF mpaka tutaposafisha kila kipande cha ardhi ya Darfur
Aug 06, 2025 08:53Rais wa Baraza la Uongozi wa Mpito nchini Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amerudia ahadi yake aliyotoa ya kuvishinda na kuviondoa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mkoa wa Darfur, magharibi mwa nchi hiyo.
-
Watu 21 waaga dunia kwa kipindupindu nchini Sudan katika muda wa wiki moja
Aug 06, 2025 03:22Wizara ya Afya ya Sudan jana ilitangaza kuwa raia wa nchi hiyo wasiopungua 21 wameaga dunia katika muda wa wiki moja baada ya kuugua kipindupindu huku maambukizo mapya yakiripotiwa kufikia 2,345.
-
MSF yasitisha operesheni katika kaunti 2 za Sudan Kusini baada ya mfanyakazi wake wa pili kutekwa nyara
Aug 06, 2025 03:21Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limesimamisha oparesheni katika kaunti mbili za Sudan Kusini kwa wiki zisizopungua sita baada ya mfanyakazi wake wa pili kutekwa nyara katika muda wa chini ya wiki moja.