Umoja wa Afrika waguswa na kuongezeka kwa fedha haramu barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i130282-umoja_wa_afrika_waguswa_na_kuongezeka_kwa_fedha_haramu_barani_afrika
Umoja wa Afrika, umeeleza kuguswa na kuongezeka kwa fedha haramu kwenye bara hilo.
(last modified 2025-09-01T07:42:49+00:00 )
Sep 01, 2025 07:42 UTC
  • Umoja wa Afrika waguswa na kuongezeka kwa fedha haramu barani Afrika

Umoja wa Afrika, umeeleza kuguswa na kuongezeka kwa fedha haramu kwenye bara hilo.

Taarifa ya Umoja wa Afrika imesema, asasi hiyo inasikitishwav na kuongezeka fedha haramu ambazo zimetokana na ukwepaji kodi, rushwa, utakatishaji wa fedha, utoroshaji wa mitaji na ufadhili wa ugaidi.

Umoja wa Afrika (AU) unakikadiria kuwa mataifa ya Afrika hupoteza zaidi ya dola za Marekani bilioni 88 kila mwaka.

Ili kukabiliana na hili, Umoja wa Afrika umechukua hatua kama vile ushirikiano baina ya Afrika na makundi ya mengine  kwa lengo la kurejesha mali zilizoibwa nje ya nchi au kuchunguza sekta zilizo hatarini kama ile ya madini.

Kadhalika nchi nyingi za Kiafrika zimeanzisha vitengo vya ujasusi wa kifedha na vitengo maalumu vya ushuru kama sehemu ya kukabiliana na sakata hilo.

Hata hivyo ripoti ya Umoja wa Afrika imeeleza kuwa, mbinu na mikakati hiyo haitoshi.

Wataalamu wanasema, hali hii imechangiwa na ukosefu wa ushirikiano baina ya nchi, mifumo dhaifu ya kisheria, lakini pia utegemezi wa viwango vya kigeni visivyoendana na muktadha wa bara la Afrika.

Licha ya bara la Afrika kuwa na utajiri mwingi lakini sera mbovu za mataifa ya bara hilo na uingiliaji wa kigeni ni mambo ambayo yameyafanya mataifa mengi ya bara hilo kushindwa kutumia vyema utajiri huo kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa wananchui wa bara la Afrika.