Ulimaji viazi ulivyobadili sekta ya kilimo nchini Lesotho
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i130320-ulimaji_viazi_ulivyobadili_sekta_ya_kilimo_nchini_lesotho
Ulimaji viazi nchini Lesotho kusini mwa bara la Afrika unapewa kipaumbele na umekuwa ishara kuu ya mabadiliko katika sekta ya kilimo ya nchi hiyo baada ya kuonekana kama chakula kikuu cha familia.
(last modified 2025-09-02T07:40:41+00:00 )
Sep 02, 2025 07:40 UTC
  • Ulimaji viazi ulivyobadili sekta ya kilimo nchini Lesotho

Ulimaji viazi nchini Lesotho kusini mwa bara la Afrika unapewa kipaumbele na umekuwa ishara kuu ya mabadiliko katika sekta ya kilimo ya nchi hiyo baada ya kuonekana kama chakula kikuu cha familia.

Mwaka 2022 , Lesotho ilichagua viazi kama zao lake linalopatiwa kipaumbele kupitia mkakati wa " Nchi moja- Zao moja la kipaumbele wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO). Mkakati huu unaashiria hatua ya ujasiri iliyochukuliwa na Lesotho kuelekea kuwepo usalama wa chakula, kustahimili hali ya hewa, na kukua kiuchumi.

Mfalme  Letsiewa Tatu wa nchi hiyo  amesema na hapa ninamnukuu. "Tuligundua kuwa kuna bidhaa tunaweza kulima Lesotho ambayo inaweza kuchangia ukuaji wa kilimo na kuleta mabadiliko katika sekta hiyo nchini. Na bidhaa hiyo ni viazi, "mwisho wa kunukuu. 

Zao la viazi hustawi katika maeneo ya milimani ya Lesotho yenye miinuko mirefu.ambayo ni makazi ya jamii nyingi zilizo hatarini. 

Chini ya mpango wa huo wa Nchi moja- Zao moja la kipaumbele wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO maeneo ya majaribio yaliyotengwa kwa ajili ya ulimaji wa viazi yameripoti mavuno ya hadi  la asilimia 20. Wakulima wachanga wanathimizwa kurejea katika kilimo huku mpango huu tajwa pia ukiandaa fursa za kilimo kwa wanawake na vijana nchini Lesotho. 

Thabo Mofosi Waziri wa Kilimo wa Lesotho amesema kuwa: "Tunazalisha tani 9,000 za viazi kila mwaka, lakini tunalenga kuongeza hadi tani 24,000 ndani ya miaka miwili. Hii itapunguza utegemezi wetu wa kuagiza bidhaa kutoka nje. Viazi si tena ni chakula kikuu tena bali ulimaji wa chakula hicho unapelekea mbee mustakabali wa kilimo wa Lesotho.