Apr 30, 2024 02:49 UTC
  • Iran na nchi za Afrika zaunda kamati ya ushirikiano katika sekta ya kilimo

Wizara ya Jihadi ya Kilimo ya Iran imetangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu na nchi za Afrika zimekubaliana kuunda kamati ya ushirikiano wa pamoja katika sekta ya kilimo.

Kutokana na hamu na ombi lililowasilishwa na mawaziri wa biashara wa Niger na Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa Iran pembeni ya mkutano wa pili wa ushirikiano wa kimataifa wa Iran na nchi za Afrika wa kutoa msaada na msukumo katika sekta ya kilimo, wawakilishi na wataalamu wa sekta tofauti nchini walibainisha fursa na uwezo wa Iran katika uga huo.
 
Vilevile, wataalamu hao walitoa maelezo kuhusu uwezo ilionao Iran katika nyanja mbalimbali za usimamizi endelevu wa udongo hususan wa tafiti za sayansi ya udongo na uzalishaji na usafirishaji wa mbolea pamoja na urutubishaji wa hali ya kibiolojia ya udongo.

Katika kikao cha pili cha ushirikiano wa kimataifa wa Iran na nchi za Afrika, kamati ya ushirikiano wa pamoja ilianza kufanya kazi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikatangaza utayari wake wa kutuma wataalamu wake katika nchi za Kiafrika na kushirikiana nazo katika utekelezaji wa miradi ya maji na udongo.

 
Mkutano wa pili wa kilele wa kimataifa wa Iran na Afrika ulifanyika Ijumaa  Aprili 26 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano uliopo katika mji mkuu Tehran, kwa kuhudhuriwa na wawakilishi katika ngazi ya maafisa wakuu wa nchi za Kiafrika wakiwemo mawaziri wa uchumi wa nchi zaidi ya 30 za Kiafrika.
 
Afrika daima imekuwa moja ya vipaumbele vya sera za nje za Iran katika kipindi cha baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.../

 

Tags