-
Tunisia yaijia juu polisi ya Ufaransa kwa kuua raia wake Marseille
Sep 04, 2025 04:06Tunisia imewasilisha malalamiko rasmi kwa Ufaransa, ikilaani mauaji ya raia wa nchi hiyo ya Kiarabu yaliyofanywa na polisi wa Ufaransa katika mji wa kusini wa Marseille.
-
Serikali ya DRC: Mwanamfalme wa Qatar atawekeza dola bilioni 21 katika sekta kadhaa
Sep 03, 2025 23:43Serikali ya Jamhuri ya Kidemokorasia ya Kongo, DRC kupitia ofisi ya Waziri Mkuu wake imetangaza kuwa, Mwanamfalme wa Qatar Sheikh Mansour bin Jabir bin Jassim Al Thani anataka kuwekeza nchini humo dola bilioni 21 katika sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo na uchimbaji madini.
-
Misri kutuma vikosi vya kulinda amani Somalia huku Ethiopia ikionyesha wasiwasi
Sep 03, 2025 09:51Misri inapanga kutuma kikosi cha kulinda amani nchini Somalia chini ya Mpango wa Msaada wa Umoja wa Afrika kwa Somalia (AUSSOM). Ingawa Ethiopia haijatoa kauli ya wazi, lakini huko nyuma ilibainisha kutoafiki ushiriki wa wanajeshi wa Misri katika kikosi hicho cha Umoja wa Afrika.
-
DRC yatuhumu waasi wa M23 kwa ukiukaji wa haki za binadamu, kujumuisha vijana kwa nguvu vitani
Sep 03, 2025 09:25Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewatuhumu waasi wa M23 kwa ukiukaji wa haki za binadamu na kuwalazimisha vijana kujiunga na harakati za kijeshi mashariki mwa nchi.
-
AU yataka mahasimu Sudan kusitisha vita ili kutoa fursa ya ufikishaji misaada baada ya maporomoko ya ardhi
Sep 02, 2025 23:03Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mohamoud Ali Youssuf, amezitaka pande zinazozozana nchini Sudan kusitisha mapigani ili kuruhusu utoaji wa haraka wa misaada ya kibinadamu kufuatia maporomoko ya ardhi.
-
Burkina Faso yapitisha sheria inayoharamisha na kujinaisha mapenzi ya jinsia moja
Sep 02, 2025 07:48Kikosi tawala cha kijeshi cha Burkina Faso kimepitisha sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja na kutangaza adhabu ya kifungo cha hadi miaka mitano jela kwa watu wote watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo hivyo vichafu. Wageni watakaopatikana na hatia pia watafukuzwa nchini humo kwa mujibu wa sheria hiyo mpya.
-
Ulimaji viazi ulivyobadili sekta ya kilimo nchini Lesotho
Sep 02, 2025 07:40Ulimaji viazi nchini Lesotho kusini mwa bara la Afrika unapewa kipaumbele na umekuwa ishara kuu ya mabadiliko katika sekta ya kilimo ya nchi hiyo baada ya kuonekana kama chakula kikuu cha familia.
-
Zaidi ya 1,000 waaga dunia katika maporomoko ya ardhi Darfur, Sudan
Sep 02, 2025 03:33Kwa akali watu 1,000 wamepoteza maisha katika maporomoko ya ardhi yaliyoharibu kijiji kizima katika eneo la Milima ya Marra magharibi mwa Sudan.
-
AU yatiwa wasiwasi na makubaliano ya mataifa ya Afrika kupokea wahamiaji wa Marekani
Sep 02, 2025 02:56Baraza la haki la Umoja wa Afrika (AU) limeelezea wasiwasi wake kuhusu makubaliano ya Washington na nchi kadhaa za Afrika, ambayo yanaruhusu nchi hizo za Kiafrika kupokea wahamiaji waliofukuzwa Marekani.
-
Zaidi ya visa 100,000 vya kipindupindu vimeripotiwa Sudan huku njaa ikishadidi
Sep 01, 2025 22:50Zaidi ya maambukizi 100,000 ya kipindupindu yameripotiwa katika nchi ya Sudan iliyokumbwa na vita katika mwaka mmoja, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA) ilisema Jumatatu.