-
Ethiopia yathibitisha kesi za kwanza za Ugonjwa wa Mpox katika mji unaopakana na Kenya na Somaliaa
May 26, 2025 02:37Ethiopia imethibitisha kesi zake za kwanza za ugonjwa wa mpox, zikihusisha mtoto mchanga wa siku 21 na mama yake, katika mji wa Moyale ulioko mpakani kusini mwa nchi, kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka za afya iliyotolewa Jumapili.
-
Kwa nini Trump anasema uongo kuhusu mauaji ya watu weupe nchini Afrika Kusini?
May 26, 2025 02:31Senzo Mchunu, Waziri wa Polisi wa Afrika Kusini amefichua uongo wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu mauaji ya wakulima wa kizungu nchini Afrika Kusini, na kusema: "Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, jumla ya mauaji sita yanayohusiana na ardhi yalitokea Afrika Kusini, ambapo watano kati yao walikuwa watu weusi."
-
Joseph Kabila kuitembelea Goma hivi karibuni
May 25, 2025 22:47Joseph Kabila Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema anapanga hivi karibuni kutembelea mji wa Goma unaodhibitiwa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.
-
Mkutano wa kuadhimisha Siku ya Afrika wafanyika Addis Ababa
May 25, 2025 07:48Mkutano wa kuadhimisha Siku ya Afrika ulifanyika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) huko Addis Ababa, Ethiopia, siku ya Jumamosi.
-
Kesi 2,500 za kipindupindu zaripotiwa chini ya mwezi mmoja mjini Khartoum pekee
May 25, 2025 03:37Waziri wa Afya wa Sudan, Haitham Mohamed Ibrahim ametangaza kuwa, wimbi kubwa la kipindupindu limeukumba mji mkuu Khartoum kiasi kwamba takriban kesi 2,500 za ugonjwa huo zimeripotiwa katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja yaani ndani ya mwezi huu wa Mei tena mjini Khartoum pekee.
-
Libya yafunga bomba la mafuta karibu na mji wa Zawiya
May 25, 2025 03:21Shirika la Taifa la Mafuta la Libya (NOC) linalomilikiwa na serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa limelazimika kufunga bomba la mafuta baada ya kugundua kupasuka na kuvuja mafuta huko kusini mwa Zawiya, yapata kilomita 45 magharibi mwa mji mkuu Tripoli.
-
Ethiopia yawapiga chanjo ya surua zaidi ya watoto milioni 11
May 24, 2025 22:50Ethiopia imeshawapiga chanjo watoto zaidi ya milioni 11 kama sehemu ya kampeni ya taifa zima ya kudhibiti ugonjwa wa surua unaoendelea kulisumbua taifa hilo.
-
Mauritius: Kurejea kwetu visiwa vya Chagos kutoka kwa mkoloni Uingereza, ni ushindi mkubwa
May 24, 2025 08:42Waziri Mkuu wa Mauritius, Navin Ramgoolam amesema kuwa, kufanikiwa nchi hiyo kuvirejesha kwenye milki yake visiwa vya Chagos kutoka kwa mkoloni Uingereza, ni ushindi mkubwa na wa kihistoria kwa taifa la Mauritius.
-
Kabila: Mfumo wa sheria wa DRC unavunda
May 24, 2025 04:17Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila jana Ijumaa ameshutumu vikali mfumo wa sheria wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati, akisema kuwa umeoza kutokana na uendeshaji mbaya.
-
Jeshi la Nigeria lashadidisha operesheni dhidi ya Boko Haram
May 24, 2025 03:32Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaangamiza wanachama 16 wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi, huku operesheni dhidi ya magaidi hao zikichachamaa.