-
Mjukuu wa Houphouët-Boigny apasishwa na upinzani kugombea kiti cha rais Ivory Coast
Apr 18, 2025 22:52Katika hatua muhimu kwenye siasa za Ivory Coast, Chama cha Kidemokrasia cha Côte d'Ivoire (PDCI), moja ya vyama maarufu vya upinzani, kimempasisha mwenyekiti wake, Tidjane Thiam, kugombea katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Oktoba 25, 2025.
-
UN yalaani mashambulizi ya RSF huko El Fasher, yatoa wito wa kuondolewa mzingiro
Apr 18, 2025 10:46Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi "ya mara kwa mara" ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) dhidi ya El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini huko magharibi mwa Sudan, likitaka kukomeshwa mzingiro wa mji huo.
-
Mawaziri wa Afya wa Afrika wazindua kampeni ya chanjo ya Polio katika eneo la Bonde la Ziwa Chad
Apr 18, 2025 10:45Mawaziri wa afya wa Afrika kutoka eneo la Bonde la Ziwa Chad wamezindua kampeni ya chanjo yenye lengo la kuwalinda watoto milioni 83 walio chini ya umri wa miaka 5 dhidi ya aina ya pili ya ugonjwa wa Polio.
-
Uganda inapanga sheria kuruhusu mahakama ya kijeshi kuwahukumu raia
Apr 18, 2025 10:12Serikali ya Uganda inakusudia kuanzisha sheria ya kuruhusu mahakama za kijeshi kuwahukumu raia kwa baadhi ya makosa hata baada ya jambo hilo kupigwa marufuku na Mahakama ya Juu.
-
Mamia hawajapatikana baada ya boti kuteketea moto, kuzama DRC
Apr 18, 2025 03:24Mamia wa watu wangali hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa na mamia ya abiria kuzama baada ya kuwaka moto katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuua watu zaidi ya 50.
-
Sudan imeingia mwaka wa tatu wa vita; wachezaji wa kikanda wana nafasi gani?
Apr 17, 2025 23:03Wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan vikiingia katika mwaka wake wa tatu, mapigano, kuhama makazi na njaa vimeifanya nchi hiyo kuwa moja ya nchi zilizotumbukia kwenye mgogoro mkubwa zaidi duniani.
-
Jeshi la Sudan: Raia wasiopungua 62 wameuawa katika shambulio la RSF jimboni Darfur
Apr 17, 2025 10:25Jeshi la Sudan leo Alhamisi limetangaza kuwa raia wa nchi hiyo wasiopungua 62 wameuawa katika shambulio la makombora la wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika mji wa al Fasher ambao ni makao makuu ya jimbo la Darfur ya Kaskazini, magharibi mwa Sudan.
-
Watu kadhaa wajeruhiwa katika maandamano ya kulalamikia kuaga dunia wanafunzi 3 Tunisia
Apr 17, 2025 10:19Watu kadhaa wamejeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika katika mji wa Mezzouna katikati mwa Tunisia kufuatia vifo vya wanafunzi watatu. Wanafunzo hao wamepoteza maisha baada ya kuangukiwa na ukuta wa shule.
-
Jeshi la Somalia laua magaidi karibu 50 wa al-Shabaab katika mashambulizi 2
Apr 17, 2025 09:19Jeshi la Somalia limewauwa magaidi 47 wa al-Shabaab katika mashambulizi mawili tofauti leo Alkhamisi, likiwemo lile la Aadan Yabaal katika eneo la Shabelle ya Kati, mji wa kimkakati uliotwaliwa na kundi hilo la kigaidi lenye mfungamano na al-Qaeda jana.
-
Kwa mara nyingine Afrika Kusini yalaani ukatili wa Israel dhidi ya hospitali huko Ghaza
Apr 17, 2025 02:12Afrika Kusini kwa mara nyingine tena jana Jumatano iliushutumu utawala wa Kizayuni kwa mashambulizi yake ya mara dhidi ya maeneo ya raia, zikiwemo hospitali za Ghaza, na kusema ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu unaofanywa na Israel.