-
Makumi wauawa katika shambulio la wabeba silaha Nigeria
Apr 14, 2025 09:38Zaidi ya watu 40 wameuawa katika shambulio la usiku wa manane dhidi ya jamii ya Zike huko Bassa, Jimbo la Plateau, huku mashambulio makali ya makundi yenye silaha yakiendelea kuripotiwa katika eneo hilo la kaskazini ya kati mwa Nigeria.
-
Mashambulio ya siku tatu mtawalia ya RSF yaua watu 450 Darfur, magharibi mwa Sudan
Apr 14, 2025 02:41Harakati ya Jeshi la Ukombozi wa Sudan, inayoongozwa na Minni Arko Minnawi (SLA-Minnawi), gavana wa jimbo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo, imetangaza kuwa watu 450 wameuawa kutokana na mashambulizi ya siku ya tatu mtawalia yaliyofanywa na wapiganaji wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) katika mji wa El Fasher, makao makuu ya eneo hilo, na kwenye kambi za wakimbizi.
-
Oligui Nguema ashinda kwa kishindo uchaguzi wa rais wa Gabon kwa kupata 90.35% ya kura
Apr 14, 2025 02:40Brice Oligui Nguema, kiongozi wa serikali ya mpito ya Gabon na mwanajeshi aliyeongoza mapinduzi ya mwaka 2023, amepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo wa 90.35% ya kura. Hayo ni kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani jana Jumapili.
-
Uhusiano na mkoloni Ufaransa wazidi kuharibika, Algeria yamwita balozi
Apr 13, 2025 22:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria imemwita balozi wa Ufaransa mjini Algiers, Stephane Romatet ili kujieleza ikiwa ni kuonesha malalamikio makali ya Algiers kuhusu kuzuiliwa balozi mdogo wa Algeria nchini Ufaransa.
-
Serikali ya DRC yalaani mauaji ya raia 52 yaliyofanywa na waasi wa M23
Apr 13, 2025 22:51Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imelaani mauaji ya raia 52 yaliyofanyika usiku wa Ijumaa hadi Jumamosi katika mji wa Goma wa mashariki mwa nchi hiyo ikisema kuwa, waasi wa M23 ndio waliofanya mauaji hayo ya umati.
-
Watu 8 wameuawa na 11 kujeruhiwa katika mlipuko wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria
Apr 13, 2025 08:48Takriban watu wanane wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa wakati basi moja katika Jimbo la Borno nchini Nigeria lilipokanyaga bomu lililotegwa ardhini na magaidi wa Boko Haram.
-
Misri: Tunatumai mazungumzo ya Iran na Marekani yatasaidia kupunguza mivutano
Apr 13, 2025 07:04Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetangaza kuwa inatarajiwa mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani yataanzisha awamu mpya itakayosaidia kuimarisha amani na kupunguza mivutano katika eneo la Magharibi mwa Asia kwa ujumla hususan Ukanda wa Gaza.
-
Mamia wauawa na kujeruhiwa katika shambulio la RSF kwenye kambi ya Zamzam
Apr 13, 2025 03:24Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan na mashirika ya misaada ya kibinadamu yamesema kuwa mamia ya watu wameuawa na kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa jana na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwenye kambi ya Zamzam ya wakimbizi wa ndani katika mji wa El Fasher, Jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan.
-
Côte d'Ivoire yaatishia kuongeza gharama za mauzo ya kakao katika kukabiliana na ushuru wa Trump
Apr 13, 2025 02:55Waziri wa Kilimo wa Côte d'Ivoire, Kobenan Kouassi Adjoumani, amesema nchi yake, mzalishaji mkubwa wa kakao duniani, inaweza kuchukua hatua ya kuongeza bei ya bidhaa hiyo iwapo mapendekezo ya ushuru wa Rais Donald Trump wa marekani dhidi ya nchi yake yataanza kutekelezwa.
-
Ni rasmi, CHADEMA haitaruhusiwa kushiriki uchaguzi ujao Tanzania
Apr 12, 2025 09:34Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (INEC), Ramadhani Kailima, amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakitaruhusiwa kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, pamoja na chaguzi zote ndogo zitakazofanyika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.