-
Sudan: RSF imeua raia wengine 32 El-Fasher, Darfur Kaskazini
Apr 12, 2025 08:09Jeshi la Sudan limesema kwa uchache raia 32 wameuawa katika shambulio jipya la Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko El-Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini.
-
Wanawake na watoto, wahanga wakuu wa unyanyasaji wa kingono DRC
Apr 12, 2025 03:05Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limesema katika ripoti yake ya karibuni kabisa iliyotolewa jana Ijumaa kwamba, kwa wastani kila baada ya dakika 30 mtoto mmoja alibakwa wakati wa mapigano makali ya Januari na Februari huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
-
Gabon wafanya uchaguzi leo; ni wa kwanza baada ya mapinduzi ya kijeshi
Apr 12, 2025 03:05Wananchi wa Gabon leo Jumamosi wanashiriki kwenye uchaguzi wake wa kwanza wa rais tangu yalipotokea mapinduzi ya kijeshi yaliyomaliza utawala wa miaka 56 ya familia ya Bongo, na kuweka mazingira ya kurejea kwenye utawala wa kiraia katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
-
UN: Katika kila nusu saa, mtoto 1 alibakwa mashariki ya DRC
Apr 11, 2025 22:49Umoja wa Mataifa umelaani kushtadi kesi za ubakaji na unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zilizoripotiwa katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu; huku makabiliano makali yakiendelea kati ya kundi la waasi la M23 na vikosi vya serikali.
-
Asasi za kiraia, wapinzani Tanzania walaani kukamatwa Tundu Lissu
Apr 11, 2025 09:02Mashirika ya kiraia, vyama vya upinzani na asasi za kutetea haki za binadamu nchini Tanzania zimekosoa vikali hatua ya kukamatwa na kushtakiwa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini humo CHADEMA.
-
Afrika Kusini yatoa mwito wa kuimarishwa mfumo wa biashara wa pande nyingi kuikabili Marekani
Apr 11, 2025 07:27Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuimarisha mfumo wa biashara wa pande nyingi ambao hivi sasa unatishiwa na siasa za kibeberu za Marekani.
-
Pande hasimu Sudan zatakiwa kulinda usalama wa raia
Apr 11, 2025 07:26Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imezitaka pande hasimu nchini Sudan kulinda usalama wa raia na kurahisisha kufikiwa na misaada ya kibinadamu maeneo ya mapigano ili kuepusha majanga zaidi ya kibinadamu nchini humo.
-
Serikali ya Sudan yakanusha madai ya kutuma mjumbe huko Israel
Apr 11, 2025 04:12Serikali ya Sudan imekanusha kwamba imetuma mjumbe Israel, kufuatia ripoti kwamba mkuu wa Baraza la Mpito la Utawala wa Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, alimtuma mjumbe kukutana na maafisa wa serikali ya Tel Aviv.
-
Ennahda ya Tunisia yataka kuachiliwa wafungwa wa kisiasa walio kwenye mgomo wa kula
Apr 11, 2025 04:10Harakati ya upinzani nchini Tunisia ya Ennahda imetoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa wanaogoma kula.
-
Reuters: Wawawakilishi wa serikali ya Kongo DR na waasi wa M23 wawasili Doha kwa mazungumzo
Apr 10, 2025 23:26Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa maafisa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wawakilishi wa harakati ya waasi ya M23 wamewasili Doha kwa mazungumzo yenye lengo la kufikia makubaliano ya kusitisha vita na kumaliza mapigano ya miezi kadhaa mashariki kwa Kongo DR.