-
M23: Hatutaki kingine ghairi ya amani nchini Kongo DR
Mar 19, 2025 23:39Muungano wa Mto Congo (AFC) na tawi lake la waasi wa M23 zinasisitiza kuwa, lengo lao kuu ni amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lakini zinadai kuwa, kufikiwa kwake kunakwamishwa na mashambulizi ya serikali.
-
Rais wa Nigeria atangaza hali ya dharura katika jimbo lenye utajiri wa mafuta, amtimua gavana
Mar 19, 2025 08:38Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ametangaza hali ya dharura katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Rivers kufuatia mgogoro wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu na utawala mbaya.
-
Rais wa Somalia anusurika jaribio la mauaji la magaidi wa al-Shabaab
Mar 19, 2025 08:23Serikali ya Somalia imetangaza kuwa mlipuko uliofanyika Jumanne mjini Mogadishu ulikuwa jaribio la kumuua rais wa nchi hiyo ambalo limetekelezwa na kundi la kigaidi la al-Shabaab.
-
Amiri wa Qatar awakutanisha viongozi wa DRC na Rwanda huku mvutano ukishadidi
Mar 19, 2025 08:20Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amewaleta pamoja viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Rwanda kwa lengo la kutuliza hali mashariki mwa DRC.
-
Afisa wa UN: Sudan Kusini iko kwenye ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe
Mar 19, 2025 04:13Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Nicholas Haysom, ameonya kwamba nchi hiyo inaweza kurejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya mapigano yaliyotokea kaskazini mashariki mwa nchi kulazimisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao, huku balozi kadhaa za Magharibi kujitolea kufanya upatanishi ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan: Mpango wa kuanzisha serikali nyingine mezaliwa ukiwa maiti
Mar 19, 2025 04:13Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Sudan amesema mpango wa makundi ya upinzani yakiongozwa na Rapid Support Forces (RSF) wa kuunda serikali nyingine nchini Sudan umezaliwa ukiwa maiti.
-
Niger yajitoa rasmi katika Jumuiya ya Nchi Zinazozungumza Kifaransa, Francophone
Mar 19, 2025 00:44Niger imejiondoa rasmi katika Jumuiya ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF) au Francophone sambamba na juhudi zinazoendelea kufanywa na taifa hilo la Afrika Magharibi za kuvunja uhusiano na kujitenga na mkoloni wake wa zamani, Ufaransa.
-
Shambulio la RSF laua raia wanne na kujeruhi wanane katika mji wa Omdurman, Sudan
Mar 19, 2025 00:43Wizara ya Afya ya Sudan imetangaza kuwa, raia wanane wameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa katika shambulizi la mizinga lililofanywa na wapiganaji wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) huko Omdurman, mji mkuu pacha wa nchi hiyo Khartoum.
-
Waasi wa M23 wakataa kushiriki katika mazungumzo ya Luanda na serikali ya DR Congo
Mar 18, 2025 07:59Mazungumzo baina ya waasi wa M23 na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), yaliyopangwa kufanyika leo Jumanne huko Luanda, mji mkuu wa Angola, yamekwama baada ya kundi hilo la waasi kusema halitoshiriki.
-
Libya yaitaka jamii ya kimataifa kuisaidia mzigo wa wakimbizi
Mar 18, 2025 07:58Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya, Emad al-Tarabelsi, ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa ukiwemo pia Umoja wa Ulaya kuisaidia mzigo wa wakimbizi haramu wanatumia ardhi ya Libya kujaribu kuelekea barani Ulaya.