-
Kikao cha mawaziri wa AU chamalizika kwa mwito wa maendeleo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii
Feb 14, 2025 09:30Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika wamemaliza Kikao chao cha 46 cha Kawaida cha Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia na kutoa mwito wa kuendelea kupigania maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii barani humo.
-
Wanajeshi wa Ufaransa kutimuliwa pia nchini Senegal
Feb 14, 2025 09:02Ufaransa na Senegal zimeeleza kuwa zimeamua kuunda tume ikiwa ni katika fremu ya maandalizi ya kuondoka wanajeshi wa Ufaransa katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Abuja yaijia juu Canada kwa kumyima 'viza' Mkuu wa Jeshi la Nigeria
Feb 14, 2025 08:40Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Nigeria, Jenerali Christopher Musa, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya ubalozi wa Canada katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, kumnyima yeye na maafisa wengine wakuu wa kijeshi viza ya kwenda Canada kuhudhuria hafla ya michezo ya maveterani wa vita huko Vancouver.
-
Ugonjwa 'usiojulikana' waua makumi ya watu DRC; mapigano yanaendelea
Feb 14, 2025 08:40Ugonjwa usiojulikana umeua watu zaidi ya 50 katika eneo la Bansakusu, jimbo la Equateur, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Utumwa na fidia ya ukoloni.. ajenda kuu za Mkutano wa Umoja wa Afrika
Feb 14, 2025 04:40Mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Afrika utakaofanyika Addis Ababa Februari 15-16, unatarajiwa kujadili masuala yanayohusiana na utumwa, ukoloni na makosa ya kihistoria yaliyofanywa na madola ya kikoloni katika bara la Afrika kwa miongo kadhaa.
-
Mali kuwaingiza jeshini wapiganaji 2,000 wa makundi yenye silaha
Feb 14, 2025 04:17Serikali ya Mali imetangaza kuwa itaanza kuwajumuisha wapiganaji 2,000 kutoka makundi washirika yenye silaha katika jeshi na vikosi vya usalama, kwa lengo la kujenga amani na harakati mbalimbali ambazo zimekuwa zikipigana dhidi ya serikali.
-
Libya, Sudan zinaongoza ajenda ya vikao vya Baraza la Amani Usalama la Afrika
Feb 13, 2025 23:45Migogoro ya Libya na Sudan imetawala siku ya tatu ya vikao vya kabla ta mkutano wa kilele wa viongozi wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, huku makao makuu ya Umoja wa Afrika yakitarajiwa kuandaa hafla ya kutiwa saini mkataba wa maridhiano kati ya pande zinazohusika katika mgogoro wa Libya.
-
Al-Azhar yaunga mkono ukarabati wa Gaza bila ya kuondolewa wakazi wake
Feb 13, 2025 23:05Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri kimetoa mwito kuungwa mkono misimamo ya Misri na mataifa mengine ya Kiarabu katika ujenzi na ukarabati mpya wa Ukanda wa Gaza bila ya kuondolewa wakazi wake.
-
OCHA: Mamilioni ya watu wameendelea kutoroka makazi yao nchini DRC
Feb 13, 2025 23:04Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema kuwa, mamilioni ya watu wanaendelea kuyahama makazi yao Kivu Kaskazini na Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Viongozi wa kanisa Kongo wakutana na waasi wa M23
Feb 13, 2025 09:05Ujumbe wa taasisi mbili za kanisa nchini Jamhuri wa Kidemokrasi ya Kongo umekutana na waasi wa M23 mashariki mwa taifa hilo katika juhudi za hivi karibuni za kusaka amani na mazungumzo baada ya wiki kadhaa za mapigano.