-
Polisi ya Nigeria yakadhibisha kutoweka maelfu ya bunduki
Feb 13, 2025 07:50Jeshi la Polisi la Nigeria limekanusha ripoti kwamba maelfu ya silaha zimetoweka kwenye maghala yake ya silaha na kuitaja rupoti hiyo kuwa ni ya kupotosha na isiyo sahihi.
-
Wanajeshi wa Ufaransa kuondoka Senegal mwishoni mwa 2025
Feb 13, 2025 07:00Ufaransa na Senegal zimeeleza kuwa zimeamua kuunda tume itakayoafanya maandalizi ya kuondoka wanajeshi wa Ufaransa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi ifikapo mwisho mwa mwaka huu.
-
Jeshi la Sudan lachukua udhibiti wa kituo kikuu cha wanamgambo wa Rapid Support Forces
Feb 13, 2025 03:21Jeshi la Sudan limetangaza kudhibiti kikamilifu mji wa Jiad, kituo kikuu cha wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) karibu na Khartoum. Mafanikio hayo yanatambuliwa kuwa ni hatua muhimu na ya kimkakati katika njia ya kulinda mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
-
Msomi wa Misri amshambulia vikali Trump, aitaka Cairo kusimama kidete dhidi ya bwabwaja zake
Feb 13, 2025 03:21Msomi wa Misri amemshambulia vikali Rais Donald Trump wa Marekani na kutoa wito wa kutolewa jibu kali dhidi ya kiongozi huyo akisema: "Lazima tusimame imara na ngangari dhidi ya Trump, na misaada ya Marekani inapaswa kupelekwa kuzimu."
-
Makumi ya wapiganaji wa ISIS wauawa katika mapigano na vikosi vya Puntland, Somalia
Feb 13, 2025 03:20Makumi ya wanamgambo wa ISIS wameuawa katika makabiliano makali na vikosi vya usalama katika eneo linalojitawala la Puntland huko Somalia jana Jumatano, huku vikosi vya usalama vikipata hasara katika mapigano hayo yaliyoanza Jumanne iliyopita.
-
Afrika Kusini: Katu hatutaondoa kesi dhidi ya Israel ICJ licha ya vitisho vya Trump
Feb 12, 2025 23:23Afrika Kusini imeapa kutoondoa kesi yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), licha ya vitisho, mashinikizo na kukatiwa misaada na utawala wa Donald Trump.
-
Kongo yapiga marufuku ndege kutoka Rwanda
Feb 12, 2025 23:22Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imefunga anga yake kwa ndege zote za kiraia na za serikali zilizosajiliwa au zile makazi yake nchini Rwanda.
-
Sudan yaafiki kuanzishwa nchini humo kambi ya jeshi la wanamaji la Russia
Feb 12, 2025 23:22Khartoum na Moscow zimekubaliana juu ya kuanzishwa kituo cha jeshi la wanamaji la Russia nchini Sudan.
-
IOM yaomba ufadhili wa dola milioni 81 kwa ajili ya Afrika Mashariki
Feb 12, 2025 05:52Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM) na washirika 45 wa masuala ya kibinadamu na kimaendeleo wameiomba jamii ya kimataifa msaada wa dola milioni 81 kwa ajili ya kuokoa maisha kwa zaidi ya wahamiaji milioni moja wakiwemo wanawake na watoto na jumuiya zinazowahifadhi katika nchi za Djibouti, Ethiopia, Somalia, Tanzania, Kenya na Yemen.
-
UN: Maelfu ya raia Kongo wahama makazi yao baada ya M23 kutoa muhula wa masaa 72
Feb 12, 2025 05:50Waasi wa M23 wanaodhibiti miji ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefunga kwa nguvu kambi za makazi za raia na kuwalazimisha zaidi ya watu 110,000 kuhama makazi yao katika siku za hivi karibuni. Haya yameelezwa na Umoja wa Mataifa.