-
Wahamiaji 27 wafariki baada ya boti kuzama mashariki mwa pwani ya Tunisia
Jan 03, 2025 04:00Wahamiaji 27 wakiwemo wanawake na watoto, wamepoteza maisha wakati boti mbili zilipozama kwenye pwani ya mashariki mwa Tunisia, huku watu 83 waliokolewa.
-
Kiongozi wa M23: Vita havitasuluhisha mzozo wa Congo, serikali ya Kinshasa inaangamiza Watutsi
Jan 03, 2025 00:13Kiongozi wa tawi la kisiasa la waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bertrand Bisimwa, ametangaza kuwa kundi lake litaendelea na mapigano katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake, mashariki mwa nchi hiyo, hadi matakwa yao ya kulindwa haki za raia wa Kitutsi na kuwahakikisha usawa kama walivyo wananchi wengine yatakapotekelezwa.
-
Wanajeshi wa Ufaransa wamefukuzwa kutoka nchi gani za Kiafrika?
Jan 03, 2025 00:13Baada ya Mali, Niger, Burkina Faso, Chad na Senegal serikali ya Ivory Coast pia inataka kuondolewa na kufukuzwa wanajeshi wa Ufaransa katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Viongozi wa Afrika watoa wito wa amani na umoja katika ujumbe wa Mwaka Mpya
Jan 02, 2025 11:02Viongozi wa Afrika wamekaribisha Mwaka Mpya kwa kutoa wito wa amani na umoja, wakilenga changamoto zinazokabili mataifa yao na kanda kwa ujumla huku wakielezea matumaini ya utulivu na ushirikiano mwaka 2025.
-
UNHCR yatoa wito wa kuwasaidia raia 3,000 wa Msumbiji waliokimbilia Malawi na Eswatini
Jan 02, 2025 04:17Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limetoa mwito wa kuwasaidia raia wapatao 3,000 wa Msumbiji waliohama nchi yao na kukimbilia nchi jirani za Malawi na Eswatini kufuatia machafuko yaliyozuka katika nchi yao baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana.
-
Rais wa Kenya akiri hadharani: Vyombo vya usalama vimejichukulia mamlaka kinyume cha sheria
Jan 02, 2025 03:18Rais William Ruto wa Kenya kwa mara ya kwanza amekiri hadharani matumizi mabaya ya mamlaka yanayofanywa na vikosi vya usalama, kufuatia wimbi la utekaji nyara wenye utata ambao umezua maandamano makubwa ya upinzani nchini humo.
-
Askari 13 DRC wahukumiwa kifo katika jitihada za kuimarisha nidhamu jeshini
Jan 01, 2025 23:11Mahakama ya kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imetoa hukumu ya kifo kwa wanajeshi 13 kwa makosa ya mauaji, uporaji, na woga katika hatua ambayo inalenga kuboresha nidhamu ya jeshi. Hukumu hizi zimetolewa Jumanne katika mji wa Lubero, Kivu Kaskazini, ambako vikosi vya Congo vimekuwa vikikabiliana na uasi hasa ule wa kundi la M23 linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda.
-
Yamkini Biya, 96, akatetea tena kiti chake urais wa Cameroon
Jan 01, 2025 23:10Rais wa Cameroon, Paul Biya, alitoa hotuba yake ya mwisho wa mwaka kwa taifa, na kutoa ishara isiyo ya moja kwa moja kwamba bado ana nia ya kuendelea kuwa rais.
-
Ouattara: Ufaransa kuondoa wanajeshi wake Ivory Coast
Jan 01, 2025 09:35Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast amesema kuwa wanajeshi wa Ufaransa wataondoka nchini humo mwezi huu wa Januari. Rais wa Ivory Coast alieleza haya jana Jumnanne katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka kwa taifa.
-
Al Burhan akataa kurejea katika mazingira kabla ya vita na kikosi cha RSF
Jan 01, 2025 09:01Kiongozi wa Baraza Kuu la Utawala la Sudan amesema ni jambo lisilowezekana kurejea katika hali ya kabla ya vita na mahasimu wao yaani wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) .