-
Katika ujumbe wa Mwaka Mpya, Ramaphosa ataka kukomeshwa vita Ghaza
Jan 01, 2025 03:09Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kwa mara nyingine tena ametoa mwito wa kukomeshwa haraka vita dhidi ya wananchi wa Ghaza. Amesema hayo kwenye ujumbe wa Mwaka Mpya aliotoa jana Jumanne.
-
Uzalishaji mafuta wastawi Angola, mwaka mmoja baada ya kujitoa OPEC
Jan 01, 2025 03:08Wastani wa uzalishaji wa mafuta kwa siku nchini Angola ulifikia mapipa milioni 1.134 katika robo tatu ya kwanza ya 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana kabla ya kujitoa kwenye OPEC.
-
Watu 1,316 wamepoteza maisha kutokana na kipindupindu tangu Agosti 12 nchini Sudan
Jan 01, 2025 03:08Takriban watu 1,316 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Sudan tangu ulipozuka ugonjwa huo katika wiki ya pili ya mwezi Agosti mwaka jana 2024.
-
SADC yataka kuhitimisha uhasama haraka iwezekanavyo nchini Msumbiji
Jan 01, 2025 00:10Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jana Jumanne ilitoa wito wa kuhitimishwa mara moja uhasama na mivutano inayoendelea huko Msumbiji ambapo watu 278 wameuawa tangu chama kikuu cha upinzani kipinge matokeo ya uchaguzi wa Rais wa mwezi Oktoba.
-
Waasi wa ADF wazidisha mashambulio mashariki mwa DRC
Dec 31, 2024 09:27Juhudi zote za jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo za kukabiliana na kusonga mbele waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo zinaendelea huku mashambulio ya waasi wenye mfungamano na kundi la Allied Defence Forces (ADF), yanaendelea katika eneo la Béni, inayopakana na Uganda.
-
Afrika Mashariki: Mjumbe wa IGAD kuzuru Sudan
Dec 31, 2024 08:08Mjumbe wa Jumuiya ya nchi za IGAD Lawrence Korbandy anatarajiwa kuzuru nchini Sudan mwezi Januari kujaribu kusuluhisha mzozo unaoendelea kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF ambao wamekuwa wakipigana tangu mwezi Aprili mwaka 2023.
-
ODM yaionya serikali ya Kenya kuhusu utekaji, yatishia kuitisha uasi wa kiraia
Dec 31, 2024 04:12Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kinachoongozwa na Raila Odinga kimetoa onyo kali, kikitishia kuongoza uasi wa kiraia dhidi ya utawala wa Rais William Ruto wa Kenya kutokana na kile kinachosema ni kuibuka siasa za kidikteta na dhuluma.
-
Serikali ya Msumbiji yaunda tume ya kuchunguza vipi jela zilivunjwa na wafungwa kutoroka
Dec 30, 2024 23:23Serikali ya Msumbiji imeunda tume ya kuchunguza tukio la kutoroka kwa wingi wafungwa kwenye vituo viwili vya magereza katika mji mkuu wa nchi hiyo, Maputo.
-
Rais wa Algeria asisitiza nia yake ya kweli ya kupambana na ufisadi
Dec 30, 2024 23:21Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria ametilia mkazo dhamira ya serikali yake ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu, na kuahidi kuanzisha mazungumzo kitaifa ili kutatua changamoto za ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu ya kaskazini mwa Afrika.
-
Afrika Kusini yaimarisha ulinzi kwenye mpaka wake na Msumbiji ili kuzuia jinai
Dec 30, 2024 08:52Afrika Kusini imeimarisha ulinzi na doria kwenye mpaka wake na Msumbiji ili kuzuia na kupambana na uhalifu nyemelezi unaoweza kujitokeza kutokana na maandamano yanayoendelea katika nchi hiyo jirani.