Watu 25 wauawa katika mapigano mashariki mwa DRC; M23 wadai kuidhibiti Goma
Zaidi ya watu 22 wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa wakati wa mapigano kati ya waasi wa M23 na vikosi vya serikali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wawakilishi wa taasisi ya kiraia na jumuiya zisizo na kiserikali katika mji wa Goma, makao makuu ya jimbo la Kivu ya Kaskazini, wameeleza kuwa mapigano yaliyoshuhudiwa tangu jana Jumatatu wiki hii yamesababisha vifo vya watu 25 na majeruhi 375.
Wakati huo huo waasi wa M23 wamedai kuuteka mji wa Goma huku raia wakikimbia mji huo.
Watu walioshuhudia mapigano hayo wameeleza kuwa bandari ya mji wa Goma imeshambuliwa na waasi wa M23 huku uwanja wa ndege wa mji huo ukiendelea kudhibitiwa na jeshi la Kongo.
Wakati huo huo, ripoti nyingine zinasema kuwa mji wa sehemu moja ya Goma inadhibitiwa na kundi na waasi huko sehemu nyingine ikiwa bado mikononi mwa vikosi vya jeshi la serikali.
Siku ya Jumatatu waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na serikali ya Kigali walidai kuudhibiti mji wa Goma huku Kinshasa ikidai kuwepo kwa wanajeshi wa Rwanda katika mji huo.
Jeshi la Rwanda pia limeeleza kuwa wanajeshi zaidi ya 120 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia nchini humo na kupokonywa silaha karibu na mji wa Gisenyi.