Wahamiaji 1,313 waliokolewa katika pwani ya Libya wiki iliyopita
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i121984-wahamiaji_1_313_waliokolewa_katika_pwani_ya_libya_wiki_iliyopita
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema kwenye taarifa yake ya jana Jumatatu kuwa wahamiaji 1,313 waliokolewa kwenye pwani ya Libya wiki iliyopita.
(last modified 2025-01-27T23:25:20+00:00 )
Jan 27, 2025 23:25 UTC
  • Wahamiaji 1,313 waliokolewa katika pwani ya Libya wiki iliyopita

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema kwenye taarifa yake ya jana Jumatatu kuwa wahamiaji 1,313 waliokolewa kwenye pwani ya Libya wiki iliyopita.

Sehemu moja ya taarifa hiyo ya IOM imesema: "Kuanzia Januari 19 hadi 25, wahamiaji 1,313 wamekamatwa na kurejeshwa Libya." 

"Wahamiaji hao ni pamoja na zaidi ya wanawake 160 na zaidi ya watoto 60," imesema sehemu nyingine ya taarifa ya shirika la IOM na kuongeza kuwa, miili ya watu wawili waliokufa maji pia imepatikana.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa wahamiaji 1,806 wamekamatwa na kurejeshwa Libya, huku wengine 32 wakifariki dunia wakiwa njiani. 

Ingawa Libya ndiyo nchi inayotumiwa zaidi na wahamiaji haramu, lakini pia ndiyo nchi yenye ukosefu mkubwa wa usalama na iliyogubikwa na machafuko tangu ulipoangushwa utawala wa kiongozi wa zamani, Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Wahamiaji wengi hasa kutoka nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara wanapendelea kuitumia Libya kufika kwenye Bahari ya Mediterania kwa ajili ya kuelekea barani Ulaya kwa tamaa za alinacha za kuwa na maisha mazuri. 

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limekuwa likitangaza mara kwa mara taarifa za kuokoa wahamiaji haramu kwenye pani ya Libya. Mwezi Septemba 2024 shirika hilo lilitangaza kuwa, limefanikiwa kuokoa wahamiaji 979 kuwarudisha nchini Libya katika kipindi cha wiki moja.

Sehemu moja ya taarifa ya IOM wakati huo ilisema: "Kuanzia tarehe 25 hadi 31 Agosti 2024, wahamiaji 979 walizuiwa kuendelea na safari za hatari na kurudishwa Libya.