-
OCHA: Watu laki tano wameathiriwa vibaya na mafuriko Msumbiji, mamba ni tishio mijini
Jan 21, 2026 07:07Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA nchini Msumbiji amesema, mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha, yamesababisha majanga makubwa kwa maisha na mbinu za kujipatia kipato nchini humo, yakiongeza pia hatari ya mripuko wa magonjwa na kuyaweka maeneo ya mijini katika hatari ya kuzingirwa na mamba.
-
Serikali ya Somalia imechukua hatua gani katika kukabiliana na kujitenga kwa Somaliland?
Jan 21, 2026 04:28Kufuatia kuongezeka harakati za watu wanaotaka kujitenga huko Somaliland baada ya kutambuliwa rasmi na utawala wa Kizayuni wa Israel, serikali ya Somalia imechukua hatua mpya za kukabiliana na harakati hizo katika eneo hilo.
-
Mahakama ya Ubelgiji yafungua tena kesi ya mauaji ya Patrice Lumumba
Jan 21, 2026 04:17Familia ya shujaa wa uhuru wa Kongo, Patrice Lumumba, ilisema jana Jumanne kwamba inatumai kupata haki, huku mahakama ya Ubelgiji ikizingatia kumfungulia mashtaka mshukiwa pekee aliyebakia hai hadi sasa kuhusu mauaji ya mwaka 1961 ya Lumumba.
-
Polisi wa Nigeria wakanusha ripoti za utekaji nyara kanisani huko Kaduna
Jan 21, 2026 04:14Polisi wa Nigeria wamekanusha ripoti kwamba waumini walitekwa nyara makanisani katika jimbo la Kaduna siku ya Jumapili iliyopita, wakisisitiza kwamba hakuna shambulio kama hilo lililotokea.
-
Afya ya kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Uganda aliyeko gerezani yadaiwa kuzorota
Jan 20, 2026 23:09Chama cha upinzani nchini Uganda cha People’s Front for Freedom kimesema katika taarifa kwamba afya ya kiongozi mkongwe wa upinzani nchini humo Kizza Besigye “iko katika hali mbaya na inaendelea kudhoofika,” na kutoa mwito wa kutaka aruhusiwe kukaguliwa na madaktari wake binafsi pamoja na familia yake.
-
Kiongozi wa zamani wa Burkina Faso akamatwa nchini Togo, anatuhumiwa kupanga njama ya mapinduzi
Jan 20, 2026 07:15Rais wa zamani wa mpito wa Burkina Faso, anayedaiwa kuwa mpangaji mkuu wa njama kadhaa za mapinduzi, amekamatwa na kufukuzwa nchini Togo.
-
Jeshi la Kongo laukomboa mji wa mashariki wa Uvira kutoka kwa waasi wa M23
Jan 20, 2026 03:47Vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vimeudhibiti tena mji wa mashariki wa Uvira baada ya waasi wa kundi la M23 kuondoka katika mji huo.
-
Naibu Mwendesha Mashtaka wa ICC: Wapiganaji wa RSF walichimba makaburi ya halaiki ili kuficha uhalifu wa kivita
Jan 20, 2026 02:03Nazhat Shameem Khan, Naibu Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), amelituhumu kundi la Rapid Support Forces (RSF) kuwa limechimba makaburi ya halaiki ili kuficha "uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu" uliofanywa katika eneo la Darfur, magharibi mwa Sudan.
-
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu Sudan
Jan 19, 2026 22:41Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu nchini Sudan huku vita vya wenyewe kwa wenyewe vikiendelea nchini humo.
-
Baraza la Katiba CAR lamtangaza Rais Faustin-Archange Touadéra kuwa alishinda uchaguzi
Jan 19, 2026 22:40Baraza la Katiba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, limetangaza mnamo Januari 19, 2026, kuchaguliwa tena Rais Faustin-Archange Touadéra kwa muhula wa tatu.