-
Balozi: Nchi 18 zimejiunga na kesi ya Afrika Kusini ICJ dhidi ya Israel
Oct 08, 2024 08:11Balozi wa Afrika Kusini mjini Tehran, Dakta Francis Moloi, ameashiria kuongezeka kwa uungaji mkono wa kimataifa kwa kesi ya mauaji ya kimbari ya Gaza dhidi ya Israel, akieleza kuwa kufikia sasa nchi 18 zimejiunga na kesi hiyo katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ.
-
Kutoka kwa hasira Rais Tshisekedi kwafunika mkutano wa kilele wa nchi za Francophone
Oct 08, 2024 02:24Hatua ya Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya kutoka kwa hasira na kususia mkutano wa nchi zinazozungumza Kifaransa (Francophone) kumeufunika mkutano huo wa kilele wa mjini Paris Ufaransa.
-
Bunge la Ethiopia lamteua Waziri wa Mambo ya Nje kuwa rais mpya wa nchi hiyo
Oct 08, 2024 02:21Mabunge mawili ya Ethiopia jana Jumatatu yalimteua Waziri wa Mambo ya Nje, Taye Atske Selassie, kuwa rais mpya wa nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika.
-
Watu 7 wameuawa, 59 wajeruhiwa katika shambulizi la makombora Sudan
Oct 08, 2024 02:19Takriban watu saba wameuawa na wengine 59 wamejeruhiwa katika shambulio lililofanywa na Vikosi vya Msaada wa Hharakati (RSF) kwenye kambi ya wakimbizi huko El Fasher, Darfur Kaskazini nchini Sudan.
-
Gachagua mashakani, Bunge la Kenya kumsaili Naibu Rais leo
Oct 08, 2024 01:12Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, leo atafahamu iwapo atanusurika au kupoteza nafasi hiyo, wakati mchakato wa kuvuliwa wadhifa wake utakapoanza huku wabunge wakitarajiwa kupigia kura hoja ya kutokuwa na imani na uongozi wake.
-
Kais Saied ashinda muhula wa pili wa urais Tunisia kwa 90.69% ya kura, vyama vya upinzani vyasusia
Oct 08, 2024 00:05Tume ya Uchaguzi ya Tunisia imetangaza kwamba Kais Saied, ambaye anahodhi mamlaka ya nchi hiyo tangu 2021, ameshinda uchaguzi wa rais kwa muhula wa pili baada ya kupata asilimia 90.69 ya kura katika uchaguzi ambao haukuwa na ushindani.
-
Mapato ya Mfereji wa Suez yapungua kwa 60% kutokana na mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza
Oct 07, 2024 23:35Mapato ya Mfereji wa Suez nchini Misri yamepungua kwa 60% tangu mwanzoni mwa 2024, wakati idadi ya meli zinazopita kwenye njia hiyo muhimu ya majini imepungua kwa 49% kutokana na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.
-
Nigeria yaipiga teke sarafu ya dola; kuanza kuuza mafuta ghafi kwa sarafu ya ndani
Oct 07, 2024 07:31Nigeria ambayo ni nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi barani Afrika, nayo imetangaza kuanza kuuza mafuta ghafi kwa sarafu ya ndani ikiwa na maana ya kuipiga teke na kuitupilia mbali sarafu ya dola ambayo inatumiwa vibaya na dola la kibeberu la Marekani kuyashinikiza mataifa mengine.
-
Mwanaharakati Nigeria: Kimbunga cha al-Aqsa kilianika udhaifu wa Israel
Oct 07, 2024 02:47Mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu nchini Nigeria amesema Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa ya Oktoba 7, 2023 iliyofanywa na wanamapambano wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ilifichua namna utawala haramu wa Israel ulivyo dhaifu sanjari na kuugutusha ulimwengu juu ya kadhia ya Palestina.
-
Somalia inatiwa wasiwasi na madai kwamba Ethiopia imetuma Puntland shehena ya silaha
Oct 07, 2024 00:20Somalia jana ilieleza kuwa inatiwa wasiwasi na hatua ya jirani yake Ethiopia ya kusafirisha silaha kinyume cha sheria katika eneo la Puntland.