Oct 07, 2024 03:50 UTC
  • Somalia inatiwa wasiwasi na madai kwamba Ethiopia imetuma Puntland shehena ya silaha

Somalia jana ilieleza kuwa inatiwa wasiwasi na hatua ya jirani yake Ethiopia ya kusafirisha silaha kinyume cha sheria katika eneo la Puntland.

Ahmed Moallim Fiqi Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia jana alizungumza na waandishi wa habari mjini Mogadishu na kuyataja madai kwamba Ethiopia imesafirisha silaha kinyume cha sheria huko Puntlandn kuwa tishio kwa usalama wa Somalia. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia ameitaka Ethiopia kuheshimu makubaliano na akapongeza jitihada za Uturuki za kuzipatanisha nchi mbili hizo jirani.

Taarifa ya awali ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia ilibainisha kuwa Ethiopia imeingiza silaha kinyume cha sheria katika jimbo la Puntland, eneo lenye mamlaka ya ndani huko kaskazini mashariki mwa Somalia.

Taarifa  hiyo iliongeza kuwa, ushahidi wa kumbukumbu umethibitisha kuwasili kwa lori mbili zenye silaha kutoka Ethiopia hadi Puntland hatua ambayo ilitekelezwa pasina ushirikiano wowote wa kidiplomasia na bila kibali.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia imesema  hatua hiyo imekiuka pakubwa mamlaka ya kujitawala Somalia na kuathiri pakubwa usalama wa taifa na kikanda.

 

 

Tags