-
Jeshi la Somalia limemtia mbaroni kiongozi mkuu wa al Shabaab
Sep 19, 2024 03:26Somalia jana ilitangaza kuwa imemtia nguvuni mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la al Shabaab katika mkoa wa kati wa Galgadud.
-
Asilimia 33 ya wagonjwa wa mpox Burundi ni watoto na vijana
Sep 19, 2024 01:13Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Burundi linasema asilimia 33 ya wagonjwa wa homa ya nyani au mpox nchini humo ni watoto wa kwenda shule wenye umri wa kuanzia miaka 5 hadi 19, na hivyo kuwa changamoto mpya wakati familia zinajiandaa kwa mwaka mpya wa masomo.
-
HRW: Makundi yenye silaha yanatekeleza mauaji Burkina Faso
Sep 18, 2024 08:00Shirika la Human Rights Watch (HRW) limesema kuwa makundi yanayobeba silaha yene mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al Qaida na kundi la kitakfiri la Daesh (ISIS) yamezidisha mashambulizi dhidi ya raia nchini Burkina Faso.
-
Malaki ya watu wa tabaka la chini Kenya wabainika kuwa na maradhi ya kisukari
Sep 18, 2024 07:47Asasi za afya nchini Kenya zimefichua kuwa Wakenya 372,000 wa tabaka la wenye kipato cha chini wamebainika kuugua maradhi ya kisukari na shinikizo la damu ndani ya miezi minne iliyopita.
-
Marekani yaondoka kabisa kijeshi Niger
Sep 18, 2024 04:35Jeshi la Marekani limetangaza katika taarifa kuwa mpango wa kuondoa wanajeshi wake katika ardhi ya Niger umekamilika.
-
Rais Samia azijibu balozi za Ulaya: Tanzania ni nchi huru, isielekezwe cha kufanya katika mambo yake
Sep 18, 2024 02:33Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amejibu matamko ya balozi zinazowakilisha mataifa mbalimbali nchini humo, yaliyotaka ufanyike uchunguzi wa haraka wa matukio ya utekaji na mauaji ya watu akisema, Tanzania ni nchi huru, hivyo haipaswi kuelekezwa cha kufanya kwenye mambo yake.
-
Raia wa Nigeria wataka kampuni kubwa ya mafuta ya Uingereza iwalipe fidia ya dola milioni 310
Sep 18, 2024 01:08Wanigeria wanataka fidia ya naira bilioni 505 (dola milioni 310) kutoka kwa kampuni kubwa ya nishati ya Uingereza, Shell, baada ya kubainika kuwa shirika hilo limechafua mazingira kwa kumwaga mafuta mara kwa mara katika eneo la Niger Delta.
-
Wanamgambo wa CODECO waua raia 10 mashariki mwa DRC
Sep 18, 2024 01:05Raia kumi wameuawa katika shambulio la usiku wa manane Jumanne lililofanywa na wanamgambo wa CODECO kwenye kijiji kimoja Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mkoa wa Ituri.
-
Amnesty International yaalaani ukandamizaji wa uhuru kabla ya uchaguzi wa rais Tunisia
Sep 17, 2024 09:29Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa serikali ya Tunisia kukomesha ukandamizaji unaoongezeka dhidi ya uhuru wa kimsingi kabla ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 6 Oktoba, 2024.
-
Milipuko na milio ya risasi yasikika katika mji mkuu wa Mali, kuna tetesi ni hujuma ya "waasi"
Sep 17, 2024 08:31Ripoti ya televisheni ya serikali ya Mali imesema kwamba "waasi wenye silaha" wameshambulia kituo cha mafunzo cha askari usalama katika mji mkuu, Bamako, mapema leo Jumanne, na kwamba hali ya mambo sasa imedhibitiwa.