Sep 19, 2024 06:56 UTC
  • Jeshi la Somalia limemtia mbaroni kiongozi mkuu wa al Shabaab

Somalia jana ilitangaza kuwa imemtia nguvuni mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la al Shabaab katika mkoa wa kati wa Galgadud.

Jeshi la taifa la Somalia (SNA) limemtia mbaroni Ali Geelle kinara wa kundi la al Shabaab aliyekuwa na mahusiano na mtandao wa kigaidi wa al Qaida katika oparesheni lililofanya katika mkoa wa Galgadud katikati ya Somalia. 

Wizara ya Ulinzi ya Somalia imeeleza katika taarifa yake iliyoituma katika mtandao wa kijamii wa X kwamba Ali Geelle ametiwa mbaroni katika wilaya ya Galhareeri katika mkoa wa Galgadud. Katika oparesheni hiyo jeshi la Sudan pia limenasa gari moja na silaha kadhaa. 

Wizara ya Ulinzi ya Somalia imeongeza kuwa kinara huyo wa al Shabaab alikuwa akijihusisha na vitendo vya unyang'anyi na tabia ya kuchukiza ya kuajiri watoto katika kufanya ugaidi.

Jeshi la taifa la Somalia huku likisaidiwa na vikosi vyake vya wanamgambo limekuwa likiendesha vita dhidi ya kundi la al Shabaab katika mikoa ya kusini na katikati ya Somalia katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita na kufanikiwa kukomboa maeneo mengi yaliyokuwa yanashikiliwa na al Shabaab ukiwemo mji wa kimkakati wa pwani wa Haradhere katika mkoa wa Mudug. 

Magaidi wa al Shabaab 

 

Tags