-
Algeria yataka kutekelezwa azimio la Baraza la Usalama la kusitisha vita Gaza
Aug 14, 2024 08:59Balozi na mwakilishi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa amelaani shambulio la Israel dhidi ya shule ya Tabeen huko Gaza na kutaka kutekelezwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kusimamisha vita huko Gaza.
-
Mahakama ya Uganda yamkuta na hatia kiongozi wa waasi wa LRA
Aug 14, 2024 04:41Mahakama nchini Uganda jana ilimpata na hatia kamanda wa zamani wa kundi la Waasi wa Kikristo la kaskazini mwa Uganda (LRA). Thomas Kwoyelo amepatikana na hatia kwa kuhusika katika makosa kadhaa ya jinai dhidi ya binadamu katika kesi ya kwanza ya jinai za kivita kusikilizwa katika nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika.
-
UN: Mafuriko yawaathiri maelfu ya watu magharibi na katikati mwa Afrika
Aug 14, 2024 04:16Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeripoti kuwa watu zaidi ya 700,000 wameathiriwa na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mabadiliko ya tabianchi mwaka huu huko magharibi na katikati mwa Afrika.
-
Afrika yatangaza 'dharura ya afya ya umma' ya Homa ya Mpox
Aug 14, 2024 00:51Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Afrika kimetangaza "dharura ya afya ya umma", kiwango chake cha juu zaidi cha tahadhari, juu ya mlipuko wa Mpox unaokua katika bara hilo, na kutoa "wito wa wazi wa kuchukua hatua" kukomesha kuenea kwake.
-
Asilimia 63 ya watoto nchini Somalia wanakabiliwa na umaskini mkubwa wa chakula
Aug 14, 2024 00:32Takribani asilimia 63 ya watoto nchini Somalia, au wawili kati ya watatu, wamepata umaskini mkubwa wa chakula katika utoto wa mapema.
-
Mazungumzo ya Sudan na Marekani yasambaratika Jeddah, matumaini ya amani yapotea
Aug 13, 2024 07:15Sudan imetangaza kufeli mazungumzo yake na ujumbe wa Marekani mjini Jeddah, Saudi Arabia, suala ambalo linazidi kupoteza matumaini ya kupatikana amani nchini Sudan katika siku za hivi karibuni.
-
Waziri Mkuu wa zamani wa DR Congo achaguliwa kuwa mkuu wa Baraza la Seneti
Aug 13, 2024 07:15Jean-Michel Sama Lukonde Kyenge, waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), amechaguliwa kuwa mkuu wa Baraza la Seneti jana Jumatatu.
-
Polisi Tanzania yawaachia kwa dhamana baadhi ya viongozi wa Chadema, wengine wakwama
Aug 13, 2024 03:22Jeshi la Polisi katika mkoa wa Mbeya nchini Tanzania limethibitisha kuwashikilia na kuwahoji viongozi na wafuasi wapatao 520 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuwaachia huru baadhi yao kwa dhamana.
-
Katibu Mkuu wa UN: Afrika inastahili kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama
Aug 13, 2024 02:10Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa mageuzi ya haraka ya Baraza la Usalama la umoja huo, akikosoa muundo wake wa kizamani na kukosekana uwakilishi kwa Afrika, ambao amesema unadhoofisha itibari ya chombo hicho na uhalali wa kimataifa.
-
Mafuriko yasababisha maelfu ya watu kuhama makazi yao magharibi mwa Ethiopia
Aug 12, 2024 23:29Takriban watu 16,000 wamelazimika kuhama makazi yao na kuelekea katika maeneo salama kutokana na mafuriko yaliyoathiri maeneo ya magharibi mwa Ethiopia.