-
Mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya Shakahola akana mashtaka ya mauaji
Aug 12, 2024 23:08Paul McKenzie, kiongozi wa kanisa la kufunga hadi kufa nchini Kenya amekana mashtaka ya mauaji ya kutokusudia kufuatia vifo vya waumini zaidi ya 400 katika mkasa unaohusiana na ibada katika pwani ya Kenya.
-
Watu 23 waaga dunia katika tukio la jaa la taka kuporomoka katika mji wa Kampala
Aug 12, 2024 09:36Idadi ya watu waliopoteza maisha yao katika janga la kuporomoka kwa jaa la takataka mjini Kampala imefikia watu 23 huku makundi ya waokoaji wakizidi kupoteza matumaini ya kupata manusura.
-
Viongozi wakuu wa upinzani Tanzania watiwa mbaroni
Aug 12, 2024 09:36Polisi ya Tanzania imemkamata mwanasiasa kigogo wa chama kikuu cha upinzani cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA, Tundu Lissu, pamoja na viongozi wengine wa chama hicho Jumapili jioni.
-
DRC na Zambia zaanza mazungumzo kufuatia kufungwa mpaka wa pamoja wa nchi mbili
Aug 12, 2024 07:21Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC ambayo ni ya pili duniani kwa uzalishaji wa madini ya shaba imesema imeanza mazungumzo na Zambia, siku moja baada ya jirani yake huyo wa kusini mwa Afrika kufunga mpaka wao wa pamoja, na hivyo kuziba njia kuu ya kusafirishia madini hayo ya DRC kupitia nchi hiyo.
-
Katibu Mkuu wa UN 'asikitishwa sana' na hali ya Sudan
Aug 12, 2024 02:58Umoja wa Mataifa umelezea wasiwasi wake Jumapili kuhusu mapigano yanayoendelea kati ya Vikosi vya Jeshi la Sudan na wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko Darfur Kaskazini.
-
Watu 28 wauawa, 46 wajeruhiwa katika mapigano mapya magharibi mwa Sudan
Aug 11, 2024 23:37Takriban raia 28 wameuawa na wengine 46 wamejeruhiwa katika shambulio lililofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko El Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini magharibi mwa Sudan.
-
Afisa wa zamani wa kikosi cha mauaji wakati wa utawala wa Jammeh atiwa nguvuni Gambia
Aug 11, 2024 07:47Jeshi la Gambia limemtia mbaroni kamanda wa zamani ambaye alidaiwa kuwa mwanachama wa 'kikosi cha mauaji" wakati wa utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Yahya Jammeh.
-
Jeshi la Sudan lathibitisha kuzima shambulizi la RSF huko El Fasher
Aug 11, 2024 07:37Jeshi la Sudan limetangaza kuwa limezima shambulio la Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwenye mji wa El Fasher, makao makuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, baada ya saa kadhaa za mapigano makali kati ya pande hizo mbili.
-
Waliokufa kutokana na mvua, mafuriko Sudan wapindukia 50
Aug 11, 2024 04:04Watu zaidi ya 50 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko katika maeneo mbali mbali ya Sudan.
-
Wahamiaji 124 waokolewa katika pwani ya Libya
Aug 11, 2024 00:52Jeshi la Walinzi wa Pwani ya Libya limetangaza kuwa limeokoa wahamiaji 124 katika pwani ya magharibi mwa nchi hiyo wakati wahamiaji hao walipokuwa wanajaribu kuvuka bahari yenye mawimbi makali ya Mediterenia kuelekea barani Ulaya.