Wahamiaji 124 waokolewa katika pwani ya Libya
Jeshi la Walinzi wa Pwani ya Libya limetangaza kuwa limeokoa wahamiaji 124 katika pwani ya magharibi mwa nchi hiyo wakati wahamiaji hao walipokuwa wanajaribu kuvuka bahari yenye mawimbi makali ya Mediterenia kuelekea barani Ulaya.
Wahamiaji hao waliokolewa karibu na eneo la Garabulli lililoko umbali wa takriban kilomita 60 mashariki mwa Tripoli mji mkuu wa Libya, baada ya mashua yao kuharibika baharini.
Walinzi wa Pwani ya Libya hawakutaja tarehe waliyofanya zoezi hilo la uokoaji lakini wamethibitisha kuwa wahamiaji hao ambao ni wa mataifa mbalimbali walipelekwa katika bandari ya Tripoli na kukabidhiwa kwa Idara ya Kudhibiti Uhamiaji Haramu.
Tangu ulipopinduliwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011 hadi hivi sasa, Libya haijawahi kuwa na utulivu wa kuendelea. Ombwe hilo la utawala limepelekea magange mengi ya magendo yakiwemo magendo ya binafamu kuitumia ardhi ya nchi hiyo kusafirisha watu kinyume cha sheria. Wengi wanaohatarisha maisha yao kwa tamaa ya alinacha ya kwenda kupata maisha bora barani Ulaya, ni vijana kutoka nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kwa upande wake, Shirika la Kimataifa la Wahajiri limeripoti kuwa, wahajiri 12,584 wamezuiwa katika katika maeneo ya pwani na kurejeshwa ndani ya Libya tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2024 hadi hivi sasa.
Cha kusikitisha zaidi ni kwamba watu hao wenye uchu wa kufika barani Ulaya wanatumia ardhi ya Libya ambayo yenye haina usalama hata kidogo. Mbali na watu hao kuishia mikononi mwa magenge hatari ya magendo ya binadamu na wengine kupingwa mnada masokoni ikama bidhaa, hali yenyewe ya usalama huko Libya nayo ni ya hatari. Hii ni kusema kuwa, watu wengine tisa wameuawa katika mapigano yaliyotokea Ijumaa kati ya makundi hasimu kwenye kitongoji cha Tajoura, mashariki mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli.