-
Kituo cha Utafiti: Haya ndiyo mambo yanayoimarisha ugaidi barani Afrika
Aug 08, 2024 07:11Kituo kimoja cha utafiti wa kiistratijia kimesema kuwa, magenge ya kigaidi yamepanua shughuli zao katika ukanda wa Sahel Afrika kwenye miezi ya hivi karibuni, na hali hii inatarajiwa kuongezeka katika miezi ijayo.
-
Waziri wa Nigeria aonya kuhusu uingiliaji wa maajinabi katika maandamano ya kupinga serikali
Aug 08, 2024 07:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Yusuf Tuggar amezitaka balozi za nchi za kigeni kuacha kuingilia maandamano yanayoendelea nchini humo, akidai kuwa serikali inafanya kazi kwa bidii ili kutatua matatizo ya raia.
-
Rais wa Tunisia amfuta kazi Waziri Mkuu na kuteua mpya
Aug 08, 2024 07:10Rais Kais Saied wa Tunisia amemteua Waziri wa Masuala ya Kijamii, Kamel Maddouri kuwa Waziri Mkuu mpya, ili kuchukua nafasi ya Ahmed Hachani, Waziri Mkuu aliyefutwa kazi na rais huyo.
-
WHO yachukua hatua dhidi ya kirusi cha Mpox huku kesi za maambukizi zikiongezeka Afrika
Aug 08, 2024 04:22Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameitisha mkutano wa dharura wa wataalamu wa kimataifa huku kesi za maambukizi ya spishi hatari zaidi ya kirusi cha Mpox zikiongezeka katika nchi za Afrika.
-
Niger yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine; uamuzi huo umeanza kutelezwa mara moja
Aug 07, 2024 23:02Niger imetangaza kuvunja mara moja uhusiano wake na kidiplomasia na Ukraine. Hayo yametangazwa na Amadou Abdramane, msemaji wa serikali ya Niger kwa njia ya televisheni.
-
Muungano wa Madaktari: El Fasher Sudan ni mahali pabaya zaidi pa kuishi duniani
Aug 07, 2024 23:01Muungano wa madaktari nchini Sudan umesema kuwa, mji wa El Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini la magharibi mwa nchi hiyo umegeuka na kuwa mahali hatari zaidi na pabaya zaidi kuishi binadamu duniani kutokana na vita vya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi.
-
Libya na Umoja wa Ulaya zajadiliana njia za kushirikiana kulinda mipaka
Aug 07, 2024 23:00Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya na Umoja wa Ulaya wamejadiliana njia za kuimarisha uwezo wa Libya katika kulinda mipaka yake.
-
Rais Tshisekedi amtuhumu mtangulizi wake kwa kuwaunga mkono waasi
Aug 07, 2024 07:50Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Joseph Kabila ameanzisha mkakati wa kuunganisha makundi yenye silaha na vyama vya kisiasa nchini humo dhidi ya serikali yake.
-
Baraza la Usalama laidhinisha MONUSCO kuipa SADC msaada wa kilojistiki DRC
Aug 07, 2024 03:13Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kuidhinisha kikosi cha kusimamia amani cha umoja huo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO kutoa msaada wa kiutendaji na wa suhula na zana za kijeshi kwa ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) nchini DRC.
-
Mafuriko kaskazini mwa Sudan yaua na kujeruhi makumi ya watu
Aug 06, 2024 23:50Shirika rasmi la Habari la Sudan (SUNA) limeripoti kuwa watu 11 wamefariki dunia na wengine 60 kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko katika mji wa Abu Hamad kaskazini mwa Sudan. Mvua hiyo imebomoa makumi ya nyumba huku timu za uokoaji zikiendelea kusaka watu waliotoweka na wengine walionasa chini ya vifusi.