Libya na Umoja wa Ulaya zajadiliana njia za kushirikiana kulinda mipaka
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i114960-libya_na_umoja_wa_ulaya_zajadiliana_njia_za_kushirikiana_kulinda_mipaka
Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya na Umoja wa Ulaya wamejadiliana njia za kuimarisha uwezo wa Libya katika kulinda mipaka yake.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Aug 07, 2024 23:00 UTC
  • Libya na Umoja wa Ulaya zajadiliana njia za kushirikiana kulinda mipaka

Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya na Umoja wa Ulaya wamejadiliana njia za kuimarisha uwezo wa Libya katika kulinda mipaka yake.

Katika mkutano huo, pande zote mbili zimesema kuwa mazungumzo na mijadala katika mkutano huo ilikuwa mizuri. Kumefanyika mapitio ya kina ya namna ya kushirikiana katika kushughulikia vipaumbele vilivyoainishwa na pande hizo mbili. 

Pande hizo mbili zimesifia matokeo chanya ya ushirikiano baina ya pande mbili na kushirikiana katika ulinzi wa mipaka ya ardhini na baharini pamoja na kupambana na uhalifu uliopangiliwa kitaasisi.

Libya na Umoja wa Ulaya zimeafanikia makubaliano ya kulinda kwa pamoja mipaka ya Libya ili kukabiliana na wimbi kubwa la wahamiaji haramu. Taasisi ya Umoja wa Ulaya ya Masuala ya Mipaka kuhusu Libya, inajulikana kwa kifupi kwa jina la EUBAM. Mwezi Mei 2013, Umoja wa Ulaya uliiruhusu EUBAM kuisaidia  Libya katika kuimarisha usalama wa mipaka yake.

Jukumu la msingi la EUBAM ni kuchangia uwezo wa serikali na mashirika ya Libya kusimamia mipaka ya nchi hiyo, kupambana na uhalifu wa kuvuka mipaka ikiwa ni pamoja na biashara ya binadamu na magendo ya wahamiaji, na kupambana na ugaidi.