-
Rais wa Zambia aidhinisha sheria ya kupanua Bunge miezi kadhaa kabla ya uchaguzi
Dec 19, 2025 03:15Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, jana Alkhamisi alisaini sheria ambayo itapanua Bunge la nchi hiyo, hatua ambayo wakosoaji wanasema inaweza kukinufaisha chama chake, miezi minane kabla ya uchaguzi wa kitaifa.
-
Jenerali Mkuu wa Sudan akutana na Rais wa Misri, vita vinaendelea
Dec 19, 2025 07:19Jenerali Mkuu wa Sudan, Abdel-Fattah al Burhan, amekutana na Rais wa Misri, Abdel-Fattah el-Sissi mjini Cairo huku kukiwa na shinikizo linalozidi kuongezeka la kuhimiza kutatuliwa mgogoro wa vita nchini Sudan haraka iwezekanavyo.
-
UN: Zaidi ya raia 1,000 waliuawa katika shambulio la RSF Darfur
Dec 18, 2025 08:22Ripoti iliyotolewa Alkhamisi na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema zaidi ya raia 1,000 waliuawa wakati kundi la waasi wa Sudan lilipotwaa udhibiti wa kambi ya wakimbizi wa ndani huko Darfur nchini Sudan mwezi Aprili mwaka huu.
-
Waasi wa M23 wamebaki Uvira licha ya kutangaza kuwa tayari kuondoka katika mji huo
Dec 18, 2025 03:55Waasi wa kundi la M23 hawajaondoka katika mji wa Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya mapema wiki hii kutangaza kuwa wataondoka katika mji huo.
-
Watu wasiopungua 12 wauawa katika shambulizi kwenye eneo la uchimbaji madini huko Plateau, Nigeria
Dec 18, 2025 03:54Takriban watu 12 wameuawa na wengine watatu kutekwa nyara baada ya watu wenye silaha kushambulia eneo la uchimbaji madini katika kijiji cha Atoso katika jimbo la Plateau nchini Nigeria.
-
Wabangladesh 32 waokolewa katika maji ya Libya
Dec 17, 2025 23:18Wahamiaji thelathini na wawili wa Bangladesh wameokolewa baada ya boti yao kuzama katika pwani ya mji wa Al-Haniya wa kaskazini mashariki mwa Libya.
-
A/Kusini yavamia kituo cha wakimbizi cha Marekani, yakamata Wakenya saba
Dec 17, 2025 23:18Kituo kimoja nchini Afrika Kusini kinachoshughulikia maombi ya visa za Marekani kimevamiwa na maafisa wa uhamiaji wa Afrika Kusini na kuwatia mbaroni raia saba wa Kenya waliokuwa wanafanya kazi nchini humo kinyume cha sheria.
-
Je, mashinikizo ya Marekani yameufanya mchakato wa uteuzi wa Waziri Mkuu nchini Iraq kuwa tata zaidi?
Dec 17, 2025 23:10Gazeti la Al-Akhbar limeandika katika ripoti yake kwamba, kuongezeka kwa mashinikizo ya kisiasa ya Marekani dhidi ya Baghdad kumeufanya mchakato wa kuunda serikali mpya ya Iraq kuwa tata zaidi.
-
Walimu 20 ni miongoni mwa watu 30 waliofariki baada ya boti kuzama DR Congo
Dec 17, 2025 09:19Takribani watu 30, wengi wao wakiwa walimu, wamefariki huku kadhaa wakiripotiwa kupotea baada ya boti kuzama katika mto ulioko jimbo la Kwilu, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Raia 104 wameuawa katika mashambulizi ya droni Kordofan Sudan
Dec 17, 2025 09:13Kwa uchache raia 104 wameuawa katika mashambulizi ya droni, ndege zisizo na rubani katika eneo la Kordofan nchini Sudan tangu Desemba 4 mwaka huu. Hayo yametangazwa na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk na kuelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka vita na mapigano kati ya makundi ya RSF na SAF huko Sudan.