-
Mke wa rais wa Guinea Bissau aliyepinduliwa akamatwa Ureno kwa tuhuma za kutakatisha pesa
Dec 17, 2025 03:08Mamlaka za nchini Ureno zimemtia nguvuni na kumfungulia mashtaka mke wa rais wa Guinea-Bissau aliyepinduliwa, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi kuhusu madai ya utakatishaji fedha. Hayo yameelezwa na polisi ya nchi hyo.
-
Takriban raia 2,000 waukimbia mji wa Heglig, Sudan baada ya kudhibitiwa na kikosi cha RSF
Dec 16, 2025 23:19Duru za habari ndani ya Sudan jana ziliarifu kuwa takriban raia 2,000 wameyaacha makazi yao katika mji wa Heglig wa magharibi mwa Sudan huko Kordofan Magharibi baada ya safari ngumu ya siku tisa ya kuhama makazi yao kufuatia kutekwa mji huo nawanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
Tanzania yaendelea kuwa chaguo la watalii wa kimataifa
Dec 16, 2025 23:19Tanzania imeendelea kushuhudia ongezeko la watalii kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya, yakiwemo Ufaransa, wanaovutiwa na uzuri wa kipekee wa asili na mandhari tofauti zinazopatikana katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
-
Bunge la Zambia lapitisha mswaada wa sheria za uchaguzi, upinzani walalamika
Dec 16, 2025 23:18Bunge la Zambia limepasisha kwa wingi wa kura mswaada wa kurekebisha vifungu vya katiba vinavyohusiana na uchaguzi ambavyo upinzani unadai vitamsaidia Rais Hakainde Hichilema katika uchaguzi wa mwaka ujao.
-
Je, mabadiliko ya mkakati wa ECOWAS yatarejesha utulivu Afrika Magharibi?
Dec 16, 2025 23:01Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) waliokutano huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria, wamelaani wimbi la mapinduzi ya kijeshi katika eneo hilo na kukubaliana kuunda kikosi cha pamoja cha kuchukua hatua za mapema za kukomesha mapinduzi na ukosefu wa usalama.
-
Mtazamo wa Tunisia na Afrika: Palestina ni jeraha kubwa zaidi la mfumo wa haki wa kimataifa
Dec 16, 2025 08:42Tunisia imeitangaza kadhia ya Palestina kuwa ni jeraha kubwa zaidi la mfumo wa haki duniani.
-
M23 yatangaza kujiondoa katika eneo la Uvira kama hatua ya kujenga uaminifu
Dec 16, 2025 08:14Kundi la waasi la Harakati ya Machi 23 (M23) lilitangaza jana Jumatatu kwamba limeamua lenyewe tu kuondoa vikosi vyake katika mji wa Uvira wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambao lilidai kuwa liliuteka wiki iliyopita na kusema kwamba, hatua hiyo imechukuliwa ili kujenga imani na kutia nguvu mchakato wa amani kati yao na serikali ya Kinshasa.
-
M23 yaendelea kuwashikilia mamia ya askari wa Burundi
Dec 16, 2025 00:36Kundi la waasi wa M23 linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda limewakamata mamia ya wanajeshi wa Burundi wakati wa mashambulizi yake ya hivi punde mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, afisa wa kundi hilo amesema, huku mapigano yakiendelea mashariki mwa DRC.
-
Mvua kubwa na mafuriko yaua watu 37 katika mji wa Safi, Morocco
Dec 15, 2025 23:22Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco leo JUmatatu imetangaza kuwa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa yamesababisha vifo vya takriban watu 37 katika mji wa pwani wa Safi nchini humo.
-
ECOWAS yapinga mpango wa mpito wa kijeshi wa Guinea-Bissau
Dec 15, 2025 23:21Viongozi wa Afrika Magharibi wamepinga mpango wa mpito uliotangazwa na watawala wa kijeshi wa Guinea-Bissau, badala yake wametaka kurejea haraka kwa utaratibu wa kikatiba. na kuonya kuhusu vikwazo vinavyolengwa dhidi ya wale wanaozuia mchakato huo.