-
UN: Mapigano yanashadidi mashariki mwa DRC
Dec 12, 2025 03:26Mapigano yanayoendelea kukithiri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yamesababisha vifo vya zaidi ya raia 70, kuwafurusha makwao zaidi ya watu 200,000 na kuwakosesha maelfu ya watu msaada wa chakula.
-
Guterres atoa wito kwa Eritrea na Ethiopia kuheshimu makubaliano ya mpaka
Dec 12, 2025 03:25Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ijumaa, amezitaka Eritrea na Ethiopia kurejea kwenye dhamira ya makubaliano yaliyomaliza rasmi uhasama kati ya mataifa hayo mawili ya Pembe ya Afrika miaka 25 iliyopita, akionya kuwa mvutano unaoibuka upya unaweza kuhatarisha amani ya eneo.
-
Sudan Kusini yatuma wanajeshi kulinda eneo muhimu la mafuta la Heglig nchini Sudan
Dec 11, 2025 23:11Sudan Kusini imetuma wanajeshi wake katika nchi jirani ya Sudan kwa lengo kulinda kisima cha kimkakati cha mafuta cha Heglig karibu na mpaka. Haya yamebainishwa jana Alhamisi na Mkuu wa jeshi la nchi siku chache baada ya Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kulidhibiti eneo hilo.
-
Watoto 100 wa shule waliotekwa nyara mwezi jana Nigeria warejea makwao baada ya kuachiwa huru
Dec 11, 2025 08:38Wanafunzi 100 wa Nigeria waliotekwa nyara mwezi uliopita katika Shule ya Kikatoliki ya St. Mary’s huko Papiri katika eneo la Gongola hatimaye wamerejea nyumbani baada ya kuachiliwa mwishoni mwa juma.
-
Waasi wa M23 wadai kuuteka mji wa kiistratejia wa Uvira, mashariki mwa Kongo
Dec 11, 2025 08:28Waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Jumatano walitoa taarifa wakidai kuuteka mji wa kimkakati wa Uvira, ambao ni kitovu muhimu cha kibiashara karibu na mpaka wa nchi hiyo na Burundi.
-
Watu 22 wafariki, 16 wajeruhiwa baada ya majengo mawili kuporomoka katika mji wa Fes, Morocco
Dec 11, 2025 02:41Watu wapatao 22 wamefariki dunia na wengine 16 wamejeruhiwa wakati majengo mawili ya makazi ya watu yalipoporomoka katika mji wa Fes ulioko kaskazini mwa Morocco, jana Jumatano.
-
Ghana yajibu mapigo kwa Israel, yawatimua wazayuni watatu waliowasili nchini humo
Dec 11, 2025 02:40Serikali ya Ghana imewatimua kwa kuwarejesha walikotoka Waisraeli watatu, katika hatua ya kujibu mapigo na kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel baada ya hapo awali kulalamikia kunyanywaswa raia wake katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion, mjini Tel Aviv.
-
Ghana yakosoa vitendo vya kinyama vya Israel dhidi ya raia wa nchi hiyo waliokwenda mkutanoni Tel Aviv
Dec 11, 2025 00:05Ghana jana Jumatano kile ilikosoa kile ilichokitaja kuwa vitendo vya "kinyama" walivyotendewa raia wa nchi hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) baada ya wasafiri kadhaa wa Ghana kuzuiliwa au kufukuzwa .
-
Rwanda yayatuhumu majeshi ya Kongo na Burundi kwa kukiuka makubaliano ya amani ya Washington
Dec 11, 2025 00:02Rwanda imeyatuhumu majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi kuwa yamekiuka usitishaji mapigano kwa mujibu wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa karibuni huko Washington kwa lengo la kuhitimisha hali ya mchafukoge mashariki mwa Kongo.
-
Wakenya watakiwa kutumia mitandao ya kijamii kuwaanika mafisadi
Dec 10, 2025 06:47Mkuu wa Utumishi wa Umma nchini Kenya, Bw Felix Koskei, ametoa wito kwa Wakenya kushirikiana na serikali katika vita dhidi ya ufisadi ambao kwa miaka mingi umeathiri utoaji wa huduma za serikali.