-
Sudan Kusini: Hatutaegemea upande wowote katika mzozo wa Sudan
Dec 10, 2025 06:44Naibu Mkuu wa Vikosi vya Jeshi la Sudan Kusini, Luteni Jenerali Johnson Olony, amesema nchi yake haitaegemea upande wowote katika mzozo unaoendelea katika nchi jirani ya Sudan.
-
Jukwaa la Afrika kuhusu wanawake, amani na usalama lafunguliwa Tunisia
Dec 10, 2025 05:36Jukwaa la Sita la Ngazi za Juu la Umoja wa Afrika kuhusu Wanawake, Amani na Usalama lilifunguliwa jana Jumanne nchini Tunisia, likisisitizia udhrura wa kuweko uratibu wa pande nyingi wa kukabiliana na changamoto za pamoja.
-
Ruto anasaka kura zaidi za Mlima Kenya uchaguzi wa 2027, ili kubakia Ikulu
Dec 10, 2025 03:04Ripoti kutoka Kenya zinasema, washirika wa Rais William Ruto wa nchi hiyo katika eneo la Mlima Kenya wamebuni mpango kabambe unaolenga kuhakikisha atapata angalau kura milioni mbili kumwezesha kurejea Ikulu katika uchaguzi wa 2027.
-
Ethiopia yakanusha kuwepo kambi za waasi wa RSF katika ardhi yake
Dec 10, 2025 02:49Ethiopia imekanusha madai ya kuwepo kambi za wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika ardhi yake, ikisema yanalenga kuibua ugomvi kati ya nchi hiyo na jirani yake, Sudan.
-
Rais wa Afrika Kusini asema uhuru wa Palestina ni njia pekee ya kutaleta amani endelevu
Dec 09, 2025 23:13Rais wa Afrika Kusini alisema Jumatatu kuwa “chochote kilicho chini ya uhuru wa Palestina na kutambuliwa kwa haki za msingi za binadamu za watu wa Palestina hakitakubalika na hakitapelekea amani ya haki na endelevu katika eneo hilo.”
-
UN: Watu 74 wamuawa katika mapigano mashariki mwa DRC, mapatano ya Trump yafeli
Dec 09, 2025 23:11Angalau watu 74, wengi wao wakiwa raia, wameuawa na 83 kujeruhiwa kutokana na mapigano ya karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mratibu wa misaada wa Umoja wa Mataifa nchini humo jioni ya Jumatatu.
-
Nigeria imewezaje kusambaratisha mahesabu ya mapinduzi nchini Benin?
Dec 09, 2025 23:05Uingiliaji wa haraka wa Nigeria kwa ombi la serikali ya Benin, ulifelisha jaribio la mapinduzi na kuzuia kuenea kwa ukosefu wa utulivu katika Afrika Magharibi.
-
ICC imemhukumu kiongozi wa Janjaweed wa Darfur kifungo cha miaka 20 jela
Dec 09, 2025 08:05Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) leo Jumanne wamemhukumu kiongozi wa wanamgambo wa Janjaweed katika jimbo la Darfur Sudan kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya ukatili katika jimbo la Darfur.
-
Kikosi kipya cha polisi wa Kenya chawasili Haiti kukabiliana na magenge ya uhalifu
Dec 09, 2025 07:59Hiki ni kikosi cha tano cha polisi wa Kenya kufika huko Haiti kisiwa kilichokumbwa na ghasia tangu kuanza kuhudumu kwa misheni ya polisi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Kenya ina polisi zaidi ya 700 nchini humo.
-
Nchi za eneo la Sahel zatishia kusimamisha ndege za Nigeria iwapo anga ya nchi hizo itakiukwa
Dec 09, 2025 07:58Shirikisho la Nchi za Sahel barani Afrika linalojumuisha Mali, Niger na Burkina Faso (AES) limetangaza kuwa litazizuia ndege zote zinazokiuka anga yashirikisho hilo kufuatia ripoti za ukiukaji wa sheria uliofanywa na Nigeria.