-
Mwanaharakati: Nchi za Afrika ziige mfano wa Kenya wa kuchunguza jinai za jeshi la Uingereza
Dec 09, 2025 03:58Uchunguzi wa bunge la Kenya kuhusu makosa na ukiukaji uliofanywa na Kikosi cha Mafunzo cha Jeshi la Uingereza nchini Kenya (BATUK) umeibua wito wa muda mrefu wa kuhoji mienendo ya majeshi ya kigeni barani Afrika.
-
Rais wa DRC aituhumu Rwanda kwa kukiuka makubaliano ya 'amani' yaliyofikiwa Marekani
Dec 09, 2025 03:56Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, ameituhumu Rwanda kwa kukiuka makubaliano ya 'amani' yaliyosimamiwa na Marekani na kutiwa saini wiki iliyopita mjini Washington DC.
-
Mlipuko wa kipindupindu DRC umeua watu 1,888, wakiwemo watoto 340
Dec 09, 2025 03:54Mlipuko wa kipindupindu mwaka huu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umeleta madhara makubwa, ukiwa na jumla ya wagonjwa 64,427 tangu mwanzo wa mwaka huu 2025, na kusababisha vifo 1,888. Watoto waliougua ni 14,818 na waliofariki dunia ni 340, na hivyo kufanya huu kuwa mlipuko mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 25 nchini humo. Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linaeleza.
-
Idadi ya waliokufa kutokana na hujuma ya RSF Kusini mwa Kordofan, Sudan, yafikia 114
Dec 08, 2025 23:10Mamlaka za Sudan katika jimbo la Kordofan Kusini zimethibitisha maafa makubwa: shambulio la ndege isiyo na rubani la waasi wa RSF lililotokea Alhamisi, Desemba 4, hadi sasa limeua watu 114 na kujeruhi 71. Miongoni mwa waliokufa wamo watoto 63 na idadi hiyo ingali inaongezeka.
-
Tinubu: Jeshi la Nigeria ‘lililinda’ Benin kufuatia jaribio la mapinduzi
Dec 08, 2025 23:09Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, amesema vikosi vya ulinzi vya nchi yake vilisaidia kulinda taifa jirani la Benin baada ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi Jumapili.
-
Ukosefu mkubwa maji unazidi kusambaa kusini mwa Somalia
Dec 08, 2025 23:08Vyanzo muhimu vya maji kusini mwa Somalia vinakauka kwa kasi huku ukame ukiongezeka, na kusababisha uhaba mkubwa kwa mamia ya maelfu ya watu.
-
Mapigano yaendelea: Makubaliano ya amani ya DRC na Rwanda yabakia kuwa ndoto
Dec 08, 2025 07:35Mapigano makali yameendelea kujiri Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakikabiliana na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na wanajeshi wa Burundi.
-
Serikali ya Tanzania yawataka wananchi wasiokuwa na dharura kubaki nyumbani Disemba 9
Dec 08, 2025 07:13Serikali ya Tanzania imewataka wananchi kusalia majumbani kesho Desemba 9, siku ambayo huadhimishwa kila mwaka kama Siku ya Uhuru wa Tanganyika.
-
DRC: M23 ikisaidiwa na jeshi la Rwanda inasonga mbele kuelekea Kivu, imeteka mji wa kimkakati
Dec 08, 2025 03:01Duru za serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimetangaza kuwa, waasi wa M23, wakisaidiwa na jeshi la Rwanda wanaendelea kusonga mbele kuelekea eneo la Kivu Kusini.
-
Serikali ya Nigeria yafanikisha kuachiwa huru watoto 100 waliotekwa nyara katika jimbo la Niger
Dec 08, 2025 02:56Serikali ya Nigeria imefanikisha kuachiliwa huru watoto 100 wa skuli waliotekwa nyara mwezi uliopita katika Jimbo la Niger. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na televisheni ya Channels Television jana Jumapili.